Shatisa Luck
New Member
- May 8, 2023
- 2
- 0
Utangulizi
Imani ya uwajibikaji ni hali ya kuamini katika ufanisi wako ili kuleta mafanikio. Kuwajibika kwa kiongozi sio hiari bali ni lazima kwa ajiri ya watu anaowatumikia. Kiongozi ni mtu yeyote mwenye sifa na anaongoza kundi au kikundi cha watu katika ofisi au jamii au nchi. Kiongozi anakuwa sio tu amebeba majukumu ya ofisi bali pia amebeba Imani za watu waliochini yake na wale anaowatumikia. Uwajibikaji hujenga Imani kwa kila mtu aliyekojuu na yule aliyekochini katika mamlaka husika. Ili mtu awajibike ipasavyo lazima mtu atambue na kuelewa mambo muhimu yafuatayo;
- Majukumu yake ya uongozi katika ofisi anayoiongoza.
- Kanuni, taratibu na mipaka ya kiutendendaji ndani ya ofisi.
- Kujenga Imani ya kiutendendaji kwa watu waliochini yake na wale waliojuu yake ili kuongeza ufanisi wa kazi na ushirikiano.
- Kujenga dhana ya uwazi kati ya mtumishi na kiongozi au kiongozi wa ofisi moja na nyingine ndani ya taasisi moja au nyingine.
- Kuondoa dhana hofu na hafifu(kujenga kujiamini) kwa watu anaowatumikia na wale wanaomtumikia hii itasaidia kuondoa mashaka ya taarifa ndani ya ofisi.
- Awe tayari kujiwajibisha kwa hiari yake mwenyewe kwa kushindwa kusimamia majukumu yake ili kuendelea kujenga Imani ya uongozi.
Mambo haya muhimu hayahitaji kufundishwa kwa kiongozi bali yawe ndio dira ya kila mamlaka husika ndani ya taasisi. Imani ya uwajibikaji haijengwi kwa maneno pekee bali vitendo kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kiutendaji. Kiongozi akiijenga Imani ya uwajibikaji pasipo upendeleo kila mtu aliyekochini na juu yake ataweza kuongeza uwajibikaji katika mamlaka husika.
Mambo muhimu yanayoongeza Imani ya uwajibikaji;
- Kuondoa dhana potofu ya kimamlaka; Dhana potofu hii ni ile hali ya kuamini ofisi zenye mianya ya fedha au mamlaka makubwa ni muhimu kusimamiwa kikamilifu kuliko ofisi zingine zilizopo nchini zinazotoa huduma au maamuzi. Kiongozi anapaswa kuwajibika pasipo kuangalia unyeti wa ofisi anayoiongoza.
- Kuondoa mamlaka ya kuteua mtu bali mtu achaguliwe miongoni mwa wenye sifa katika ofisi au taasisi husika katika kuongoza ofisi husika au mamlaka Fulani; Imani ya uwajibikaji inajengeka katika ukweli na uwazi katika wengi. Uteuzi unaibana sana Imani ya uwajibikaji kwa wengi kwani inasaidia tu kwa aliyemteua kutimiza majukumu yake na sio kuwajibika katika uongozi aliokabidhiwa. Bali mtu akichaguliwa katikati ya miongoni wenye sifa inajenga Imani ya kuweza kuwajibika kiuongozi na sio kwa mamlaka ya mtu au kiongozi fulani.
- Kuweka uwiano katika elimu; Elimu katika kuongoza ni muhimu sana kwa kila kiongozi. Imani ya uwajibikaji inachangizwa na elimu katika kufanya maamuzi ndani ya ofisi. Ni ngumu mtu kuwajibika bila kujua kujipima ufanisi wa uongozi wake yeye mwenyewe. Kunatakiwa kuwe na kiwango cha elimu aliyofikia mtu ili awe kiongozi hii inasaidia kujipima ufanisi wake yeye mwenyewe ili kuweza kuhimili uongozi wake.
- Uzoefu wa kimaamuzi katika uongozi au utumishi wake; Imani ya uwajibikaji inajengwa na uzoefu wa kufanya maamuzi magumu na yenye tija katika ofisi au Taifa. Mtu mwenye uzoefu wa kuamua kipi kifanyike na kipi kisifanyike kwa wakati huo ndio mwenye uwezo wa kuwajibika kwa manufaa ya ofisi au taasisi. Uzoefu huu unatokana na watu wenyewe waliondani ya ofisi au taasisi anayoitumikia na sio nje ya taasisi husika.
- Kuweka mipaka ya kiutendendaji katika ofisi na hisia za kisiasa; Imani ya uwajibikaji inajengwa zaidi na mipaka kati ya kiongozi mtendaji na kiongozi msimamizi. Huwezi kuwajibika ipasavyo kama mtu anaingilia utendaji wa mtu pasipo na mipaka. Mipaka ikiwekwa na kuzingatia inaongeza uwajibikaji katika ofisi.
Mambo yafuatayo yanaathiri imani ya uwajibikaji katika ofisi au taasisi;
- Siasa zisizo na staha katika shughuli za kiutendendaji; wanasiasa wanapofuata mipaka yao ya uongozi na utendaji katika kutekeleza majukumu yao wanasaidia kuongeza Imani ya uwajibikaji katika ofisi baina ya kiongozi wa kisiasa na mtendaji wa shughuli za ofisi au mamlaka. Kunapokuwa hakuna staha katika kufuata kanuni na taratibu za maonyo au uwajibishaji kati ya mamlaka ya juu na kiongozi inavuruga Imani ya uwajibikaji.
- Matamko yasiyofuata kanuni na taratibu katika taasisi; Imani ya uwajibikaji inaporomoshwa na matamko yasiyofaa kutoka kwa kiongozi anayesimamia mamlaka au taasisi. Kunapotokea matamko ya uzushi au Hira au njama ili mtu akwame katika shughuli au jambo muhimu kuna shusha Imani ya mtu kuwajibika ipasavyo na pia inamfanya kuwa na hofu katika majukumu yake.
- Mawazo potofu ya kushika nafasi ya mamlaka; Imani ya uwajibikaji inaathiriwa na dhana hii hasa katika nafasi za kiteuzi katika mamlaka. Kiongozi anashindwa kuwajibishwa kwa sababu za kiteuzi na pia usimamizi unadhorota zaidi kwani tayari anaimani na aliyemteua na sio kutimiza majukumu yake ya uongozi katika kuwajibika kwa anaowatumikia.
- Hofu ya kukosa mamlaka; Imani ya uwajibikaji inaathirika katika hofu ili kuondoa hofu hii ni kusimamia Imani ya kuwajibika katika majukumu ya uongozi katika ofisi au taasisi. Mtu anapokuwa na imani ya uwajibikaji kwa kila jukumu lake la uongozi huondoa hofu ya kukosa mamlaka hasa wakati akitimiza majukumu husika. Ili kuondoa hii hali kiongozi awajibike pasipo kuweka wazo la mamlaka aliyopewa bali azingatie kanuni na taratibu za taasisi katika maagizo ya kimamlaka hii itaondoa upendeleo katika upande mmoja na kuongeza ufanisi wa kiongozi.
Hitimisho; Imani ya uwajibikaji inajengwa kwa kufuata misingi ya kanuni na taratibu za uongozi katika Mamlaka au ofisi kwa kutoa maelekezo yenye uwazi.
Imani ya uwajibikaji inatakiwa ijengeke kwa kila kiongozi ili kuacha nyenzo za kuwajibika kwa wale anaowaongoza.
Kumbuka kila kiongozi akiijenga Imani yake katika kuwajibika kunamfanya kuwa huru hata akikutana na changamoto za kiuongozi katika taasisi,idara au ofisi katika kutimiza majukumu yake.
Upvote
1