vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Sioni sababu za kufanya unabii, maana unaweza ukajikuta unajicontradict. Unasema sababu ya kuipa nafasi Yanga ni consistency (maana yake muendelezo wa matokeo mazuri katika michuano husika),ndio nikakwambia, kama kigezo ni consistency basi Simba is more consistent than Yanga, kwa kuwa katika michuano yote hiyo tangu raundi za awali, Simba imepoteza mechi moja tu, ambayo ni away dhidi ya Wydad, while Yanga amepoteza mbili, Belouzdad 3-0 na Ahly 1-0. Labda ubadilishe kigezo
1) umeangalia kupoteza ila hukuangalia kushinda mechi ngapi. Simba imeshinda mechi mbili tu katika mashindano ya kimataifa msimu huu. Imemfunga Galaxy na Wydad pekee.
2) Simba mara nyingi hapa ndio huwa meisho wake hivyo kama consistency labda ya kucheza robo fainali ambapo safari hii wapo pamoja na Yanga.
3) Yanga msimu uliopita alicheza fainali mashindano ambayo mliyoyabeza na mkitegemea hatofika mbali klabu bingwa ila kafika mnapofika nyie, mpaka hapo tayari kawa na muendelezo mzuri wa mashindano ya CAF hivyo anatafuta record ya kucheza fainali za CAF mara mbili mfululizo huku safari hii ikiwa ni mashindano yenye hadhi zaidi.