Imani Yetu Kuhusu Uwepo wa Mungu Inakiuka Uwezo Wetu wa Kufikiri Katika Kupatia!!!

chige

At the risk of sounding pompously self congratulating and uppity.

Kwa mtu aliyesoma statistics na kujua standard /bell curve/ normal distribution ataelewa umeandika nini hapo.

Na kwa nini napata tabu sana kuelezea Mungu hayupo, kwa sababu nabishana na majority iliyo chini ya bell curve.
 
Ahsante sana. Karibu kwenye upagani.
 
Wawakilishi kwa maana ipi? Kwa sababu hata hao viongozi wa imani hawana cha ziada zaidi ya kuwa na elimu ambayo hata asiye kiongozi anayo elimu hiyo.

Ndiyo maana nikasema tatizo sio kuhoji bali hakuna huyo wa kujibu hizo hoja.
Mtu kama kaamka na kusema kaota kuhubiri hata ukimuuliza swali atakujibu kipuuzi!.. Lakini waliosomea Theology halafu ukamuuliza atakujibu kwa kuridhika kwako!.
Wa kuwahoji wapo, tatizo hujui kuwatafuta!.
 
Mtu kama kaamka na kusema kaota kuhubiri hata ukimuuliza swali atakujibu kipuuzi!.. Lakini waliosomea Theology halafu ukamuuliza atakujibu kwa kuridhika kwako!.
Wa kuwahoji wapo, tatizo hujui kuwatafuta!.
Kwa uelewa wangu mkuu huku kusema kwamba masuala ya Mungu hayapaswi kuhojiwa,huja pale watu wanapotaka kuhoji vitu ambavyo hatuna elimu navyo. Kuna mambo ambayo hatuyajui kwa sababu hatuna elimu nayo,na ndiyo hapa nilipopakusudia mimi na ndiyo nikasema hakuna wa kuhojiwa hayo masuala.

Kwahiyo yale ambayo tuna elimu nayo wapo wa kwenda kuwauliza,ila zaidi ya hapo huko ndiyo nadhani penye makatazo.
 
Kwa imani yangu ya kikatoliki swali lolote naweza mhoji padre/paroko na akalijibu nisichoruhusiwa ni kukashfu tu!.
 
Ahsante sana. Karibu kwenye upagani.
Kwangu kuhoji uhalali wa imani hakuna uhusiano wowote na upagani!! Najua kwenye hizi dini zetu tunaambiwa tusihoji lakini siamini, kama kweli Mungu yupo, basi alitaka aaminiwe na misukule!!!

Haya ya eti kuhoji ni kufuru mbele za Mwenyezi Mungu ni janja janja tu ya wanadamu waliofahamu in advance kwamba watashindwa kujibu baadhi ya hoja za waumini na hivyo kuhatarisha maslahi yao ya kuhudumu kama kiongozi wa dini!!!
 
Tumetishwa, tukatishika kwamba, ukihoji ni kukufuru na adhabu ya kufuru ni kubwa... JAHANAMU!!
 
Mimi nasoma biblia lakini sijaona Mungu kakataza kumhoji, Isaya 43:26 unikumbushe na tuhojiane, eleza mambo yako upate kupewa haki yako.

Mungu katoa ruksa kumhoji kwa lengo la kufaham ili tusiwe na mashaka mioyoni, shida tunayowauliza hao viongozi was dini wao pia hawayajui hapo lazima wakusukumie issue ya kukufuru.
Kwa kifupi hatujui mengi hata Yesu alilisema hilo "bado nikali ninayo mengi ya kuwambia lakini nikiwambia sasa mtaburst vichwa(mtakua machizi). Ndo maana kuna level za kujifunza level one, level two till advanced one, hivyo kaa mbele za Mungu anza kuuliza na kuhoji yeye anajua namna atakavyokuletea majibu ya matamanio ya moyo wako.
 
Unaona sasa... "Mungu ametoa ruksa ya kumhoji kwa lengo la kumfahamu..."

Ukiangalia hiyo sentensi ni kwamba, mosi unatakiwa kuamini kwanza uwepo wake na ndipo uhoji hili na lile ili upate kumfahamu vizuri! Na hata ukienda kwenye Imani 12 za Kikristo, ya kwanza kabisa ni kuamini uwepo wa Mwenyezi Mungu.... na ndivyo ilivyo kwa Waislamu na Wayahudi.

Kwa maana nyingine, as long as wewe ni Mkristo, tayari unakuwa umeshaamini uwepo wa Mwenyezi Mungu! Na kama umeshaamini, huwezi tena kuhoji uwepo wake!
 
Napata kigagaziko. Kwa muktadha wa Sasa magu regime seems not be accepted by the majority, so does to say he is right!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…