Imani za kishirikina haziwezi fua dafu ukiwa unatoa fungu la kumi, Je hivi ni kwanini?

Imani za kishirikina haziwezi fua dafu ukiwa unatoa fungu la kumi, Je hivi ni kwanini?

KWA TABU NILIYO PATA NA KANISA HAKUNA LILICHO NISAIDIA

WAKAJA KUNISAIDIA WATU WENGINE AMBAO HATA KANISANI HUWA HAWAFIKI

HAPO NDIPO NILIPO FAHAMU NINI MAANA YA UPENDO NA NDIPO NILIPO BADILI MAAMUZI

FUNGU LA KUMI LANGU NITAMNUNULIA HATA MPIGA DEBE MSOSI STENDI
Huo ndio ukweli,huko makanisani wamejaa matapeli tu, bora kuwasaidia msikini moja kwa moja
 
Shida si fungu la Kumi, shida ni nani anayepasa kukusanya na kugawa hiyo mali!
Kuna tofauti kati ya zaka na sadaka. Kwenye uislam ni roughly 2.5% ya mali iliyopituka mwaka. Na Kuna maelekezo nani akusanye na nani anufaike!

Kwenda kuwapa hawa matapeli wa mjini Wakina Kiboko ya Wachawi ni afadhali uigawe mwenyewe kwa wajane, mayatima, wasafiri namwenye shida wengine!
 
MUNGU AMEAHIDI KUWABARIKI WANAOTOA SADAKA(ikiwemo kutoa zaka na kuwasaidia wajane,na wasiojiweza,maskini,yatima,wanyonge)
s
ufalme wa giza nao unapokea kafara sadaka ili kusaidia watu wao,hakuna cha bure sadaka inahitajika katika ufalme wa giza na nuru,hata free manson huwa wanatoa sana misana,kuna kafara za misaada ,zawadi ,hata mchawi anaweza kukupa zawadi au chakula ili akudhuru akufanyie uchawi kukudhuru,hakuna cha bure
 

Attachments

  • images - 2024-09-25T200740.377.jpeg
    images - 2024-09-25T200740.377.jpeg
    37.7 KB · Views: 2
It true 100%
huu ulimwengu una watu makatili sana (washirikina, walozi na wachawi) they dont care about you even 1%
Siyo tu kwenye biashara hata kwa mfanyakazi, atoe 10% kwenye mshahara wake.
Sijui nitoe ushuhuda!
Toa mkuu, utafundisha wengi
 
Nimesikia kua ukiwa na biashara fulani ukatolea zaka mtaji wako na baada ya hapo ukawa mwaminifu kulipa fungu la kumi katika faida unazovuna.. hapa UTAKUA UMEMALIZA MZIZI WA FITINA WA CHUMA ULETE. hivi hii inabe applied kwa vipi wabobezi wa imani naomba ufafanuzi.
Acha dhambi ndio salama yako,fungu la kumi ukitoa halafu unaishi kwenye dhambi hiyo hela ni sawa na kuitupa,hakuna thawabu yoyote utakayopata hapo...
 
Sheria inayoto govern juu ya matoleo ni hii

2 Kor 9:6-15​

2 Kor 9:6-15 SUV​

BHNSUVNenoSRUV
Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu; mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote. Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu. Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo.
Anayelinda mali,afya Yako ni Yesu na si fungu la kumi.
 
1.SHERIA/KANUNI YA KUMILIKI MALI HAPA DUNIANI NI KUPITIA KUTOA(sadaka ,kusaidia wahitaji/maskini/yatima,wajane ,wasiojiweza ,wagonjwa,wanyonge,vilema,wafungwa n.k
Kadiri unavyotoa kwa wingi ndivyo unavyopokea kwa wingi.(Hii ni kwa wote uwe na dhambi ,usiwe na dhambi,uwe mpagani ,au mtu wa dini)
mfano CORNELIO alikuwa mtoaji mzuri aana hata kabla hajamjua Mungu,na sadaka zake zilipokelewa
kuna wapagani lakini wanatoa sana misaada kwa masikini na wanabarikiwa kupitia kutoa kwao kuliko hata watu wenye dini lakini ni wachoyo kutoa.
2)KANUNI YA KUMILIKI /KURITHI UFALME WA MUNGU/ MBINGU AU KUINGIA MBINGUNI NI KUWA MTAKATIFU( kuacha dhambi zote kwa 100% UTAKATIFU.)
kuna wapagani wamebarikiwa sana kwa sababu ya utoaji lakini kama hawataacha upagani na kuacha duambi kuutafuta UTAKATIFU mbinguni hautaweza kiingia kama sinmtakatifu,ila duniani unaeeza kumiliki mali kwa kufuata kanuni za kumiliki,mojawapo ni kutoa sadaka na kusaidia masikini,nyingine ni KUFANYA KAZI,Kwa bidii na kwa maarifa.
 
Hapana watu wanasisitiza kua ni kweli mkuu chunguza vizuri
Wanaosisitiza ni wanufaika wa hiyo hela, kwa sababu msipotoa watakula wapi? Chakula cha mungu ni sala, na chakula cha binadamu ni fungu la kumi, michango na sadaka.​
 
Nimesikia kua ukiwa na biashara fulani ukatolea zaka mtaji wako na baada ya hapo ukawa mwaminifu kulipa fungu la kumi katika faida unazovuna.. hapa UTAKUA UMEMALIZA MZIZI WA FITINA WA CHUMA ULETE. hivi hii inabe applied kwa vipi wabobezi wa imani naomba ufafanuzi.
Mungu ana kanuni zake na ziko wazi, hakuna Short cut, unataka Short cut, jaribu Kwa SHETANI.
 
Nina mengi ila nakupa ushuhuda mdogo sana.
Nilikuwa na madeni ambayo chanzo chake ni uchawi/roho ya chumaulete. Coworkers nao ni washirikina na wamepigana kuniharibu, na taarifa zote napata kupitia ndoto/ulimwengu wa roho ambazo ni za uhalisia, na mwishowe kupata matokeo yake ktk ulimwengu wa mwili. I was suffer kinyamaaa!
Uzuri nilikuwa natoa taarifa kwa kulalamika kwa mchungaji na viongozi wengine wa dhehebu langu, so mchungaji akanishauri kuvunja madhabahu walizojenga maadui zangu kwa kutoa sadaka. Baada ya hapo akanishauri kuanza kutoa 10%. Imagine nina madeni na ninapaswa kutoa 10%! Ni ngumu sana mzee ila ilinibidi nitumie imani ya KIMUNGU, nilitoa 10% kabla sijatumia pesa yoyote ktk mshahara wangu even kulipa deni! Guess what happen? Baadhi wafanyakazi wenzangu wakaanza kunikwepa na mwingine kuniita mchawi na mambo maovu yakaanza kuwarudia wao.
Ameen
 
Nimesikia kua ukiwa na biashara fulani ukatolea zaka mtaji wako na baada ya hapo ukawa mwaminifu kulipa fungu la kumi katika faida unazovuna.. hapa UTAKUA UMEMALIZA MZIZI WA FITINA WA CHUMA ULETE. hivi hii inabe applied kwa vipi wabobezi wa imani naomba ufafanuzi.
Fungu la kumi lenyewe ni imani ya kishirikina iliyovikwa utakatifu wa Mungu asiyethibitishika.
 
Acha dhambi ndio salama yako,fungu la kumi ukitoa halafu unaishi kwenye dhambi hiyo hela ni sawa na kuitupa,hakuna thawabu yoyote utakayopata hapo...
Kuna binadamu ambaye Hana dhambi? Na ndio mana sadaka lazima utoe
 
Back
Top Bottom