Imejitokeza sintofahamu ya watoto kupotea na kukutwa wakiwa wamefariki huku miili yao ikiwa haina baadhi ya viungo, mamlaka ichuke hatua stahiki

Imejitokeza sintofahamu ya watoto kupotea na kukutwa wakiwa wamefariki huku miili yao ikiwa haina baadhi ya viungo, mamlaka ichuke hatua stahiki

Southern Giant

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
621
Reaction score
1,298
Wakuu amani ya Mungu iwe nanyi.

Kumekua na taharuki kwa wakazi wa Temeke, Tandika, Mbagala na Vikindu kwa ujumla wake.

Imejitokeza sintofahamu ya watoto kupotea na kukutwa wakiwa wamefariki huku miili yao ikiwa haina baadhi ya viungo.

Majuma kadhaa yaliyopita maeneo ya Mbagala Mgeni nani miili ya watoto imekutwa huku baadhi ya viungo vikiwa havipo.

Pia soma: Ukatili: Mtoto auawa na kukatwa sehemu za siri

Wiki iliyoisha maeneo ya Tandika mtoto wa jirani yangu alikoswa kuchukuliwa na watekaji mara baada ya kufanya jaribio la kumteka mtoto, bahati nzuri mtoto alikimbia na kuja kusimulia kwa wazazi wake.

Juzi maeneo ya Kisemvule inaripotiwa mama mjamzito amekutwa amefariki huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.

Jana maeneo ya vikindu(kazole) nimepewa taarifa ya kukutwa kwa miili ya watoto wawili wanaodaiwa kuwa na miaka kati ya 11 mpaka 14 ikiwa haina baadhi ya viungo.

Vyombo vya habari mpaka sasa sijasikia ikiripoti tokio lolote kati ya hayo juu au yanayo shaabiana na hayo.

Rai yangu kwa mamlaka husika tunaomba wanaotenda haya matukio muwashughulikie haraka sana watatumalizia watoto wetu na jamaazetu.

MUENDELEZO WA TAARIFA ZILIZONIFIKIA MUDA HUU 19/7/2024:

Jana vingunguti wamekutwa watoto wanne wamefariki huku baadhi ya viungo na sehemu zao za siri zikiwa hazipo (zimenyofolewa).

Mbali na vingunguti pia maeneo ya ulongoni kunamtoto wakiume amepotea mpaka sasa hajapatikana

====

Pia soma: Kagera: Mwanafunzi auawa, mwili watupwa kichakani
 
Ilitokea mara kadhaa, kuna siku alikamatwa mmoja badala wenzake kukimbia, bahati mbaya raia wakamuua haraka, angeachwa hai angasaidia uchunguzi.
shida hao wasiposhughulikiwa mtaani wakienda polisi baada ya mwezi unasikia ametoka alafu hakuna hata mtu mwengine atakaye kamatwa kupitia huyo mhalifu, bola wauwawe tu
 
Back
Top Bottom