Wakuu amani ya Mungu iwe nanyi.
Kumekua na taharuki kwa wakazi wa Temeke, Tandika, Mbagala na Vikindu kwa ujumla wake.
Imejitokeza sintofahamu ya watoto kupotea na kukutwa wakiwa wamefariki huku miili yao ikiwa haina baadhi ya viungo.
Majuma kadhaa yaliyopita maeneo ya Mbagala Mgeni nani miili ya watoto imekutwa huku baadhi ya viungo vikiwa havipo.
Wiki iliyoisha maeneo ya Tandika mtoto wa jirani yangu alikoswa kuchukuliwa na watekaji mara baada ya kufanya jaribio la kumteka mtoto, bahati nzuri mtoto alikimbia na kuja kusimulia kwa wazazi wake.
Juzi maeneo ya Kisemvule inaripotiwa mama mjamzito amekutwa amefariki huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.
Jana maeneo ya vikindu(kazole) nimepewa taarifa ya kukutwa kwa miili ya watoto wawili wanaodaiwa kuwa na miaka kati ya 11 mpaka 14 ikiwa haina baadhi ya viungo.
Vyombo vya habari mpaka sasa sijasikia ikiripoti tokio lolote kati ya hayo juu au yanayo shaabiana na hayo.
Rai yangu kwa mamlaka husika tunaomba wanaotenda haya matukio muwashughulikie haraka sana watatumalizia watoto wetu na jamaazetu.