Habarini ndugu zangu.
Hivi karibuni nimepata wakati mgumu sana baada ya kupata rafiki (mwanaume mwenzangu) ambae aliniomba nimsaidie jambo flani na urafiki ukaanzia hapo.
Huyu jamaa alianza mazoea ya kunitembelea geto na akawa anapenda kunisogelea karibu sana hata tukiwa tumekaa pamoja, alianza tabia ya kunisogezea mikono ila alipoona nakereka akaacha mwenyewe.
Kinachonipa hofu ni tabia yake ya mara kwa mara kuniambia ananipenda kila anaponipigia simu tena kwa sauti laini sana wakati wa kuhitimisha mazungumzo.
Hii inakua vipi wadau?
Msaada wa mawazo tfdhl.