Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
Mkuu Kuna sehemu lazima uwe mbabe kidogo Ili kurinda uanaume wako.Ni sawa mkuu, lakini wasifanye hiyo biashara ni lazima kwa kila mtu.
Nilienda kunyoa baada kumaliza wakaniambia hamia pale.akili ikaniambia hapa Kuna Hela utaacha.
Nikahamia alipo sema mara mdada huyu hapa akaaza kusema uso wako unamafuta naweza kukufanyia..... Nikamwambia ni wewe tu akakomaaa wee alipomaliza akaniambia vipi kuhusu kupa black nikamwambia hiyo hapana. Bahati nzuri Hela ilikuwa ya chenji nikaenda Kwa kinyozi nikampa 3000 yake halafu akauliza kule mmeshamalizana?
Nikamjibu wapi Tena boss? Akamuita yule dada akasema aache 2000 ya kwangu nikamwambia mlinambia wapi? Mimi nimeuliza mkasema kunyoa ni buku3 asee tusisumbuane huku na huku nikamwambia sitoi Hela nyingine Mimi nilijua huduma hizo zingine ni offer muwe mnasema kabla hujafanya ...yule dada alinifyonza Hadi Leo sijawahi fyonzwa vile asee... Nikaenda baada ya wiki nikaendapo Tena nikamkuta yule dada ......