Siku hizi ktk kanisa katoliki tunasalimiana hivyo kama ishara ya kutakiana amani na heri, zamani kabla ya korona tulikua tunapeana mikono, baba askofu alimwinamia mh rais Samia kama ishara ya kumkaribisha nyumbani kwake na kumtakia amani awapo mahali pale, rais alitakiwa kujibu kwa kuinama pia kuonesha amepokea, nadhan sio utamaduni wake (mama) Wala wa dini yake, ndo maana alifunga mikono na bila shaka alitamka maneno fulani ya kuonesha ameitikia salamu, hapo hakuna kosa kutoka upande wowote ule, kila mtu alifanya kile kilichopo ktk mazingira yake, Imani yake na nafsini mwake, kufanya tofauti na unachokiamini ndio kosa. Asante mama kwa heshima uliyompa mzee kwa kuacha majukumu yako yote ya kitaifa na kimataifa ukaenda kijijini ngara kushiriki shughuli hiyo muhimu, hakika umemheshimisha sana mzee na umeliheshimisha kanisa katoliki, sasa panga na safari ukamsalimie baba mtakatifu Francis kama wenzako wote walivyofanya ukimwacha mtangulizi wako.,Asante sana Mama.