Imekuwaje Mkataba wa Amani kati ya Congo na Rwanda, Tanzania tumewekwa kando?

Trump hataki shobo
Hata kwenye vita yukrain, anaenda kuongea na putin, hamuiti zeleski
Uganda ndio mfadhili wa Rwanda, yeye hakuitwa , kwanini Tanzania wanashawa kuitwa,?
mbona wewe mbishi hivi, unaambiwa Ugandan president alialikwa akatuma mwakilishi wake ambae ni Vice president Jessica Alupo bado umeshupaza shingo, ukiwa hujui kitu usiwe mbishi, uwezo wako wa kufikiria unapoishia wa wenzako ndiyo unaanzia hapo
 
Rais wenu hatambuliki, alifikiri akitangazwa na tume yake ndio atatambulika.
 
Nikiwahi kusoma mahali!

"Amani ikipatikana Congo,yanayotokea Congo ndio yatatokea Tanzania"

Kuna dalili ya wazi kabisa kwamba siasa za Sasa zinaenda kuzalisha makundi ya waasi nchini na wizi wa rasilimali utaanza rasmi nchini!

Inasemekana Kwa utajiri hapa Africa Congo ni ya kwanza kirasilimali na Tanzania ni ya pili!

Sasa kama Congo amani inapatikana basi mabeberu yatahamia Tanzania ku destabilize!!!

No reforms no election imetufikisha huku na mwito wa maandamano ndio lango la Congo mpya ya machafuko ndani Tanganyika!

Nawaza,nipo tayari kukosolewa comrades!
 
Unamaanisha rasilimali kwa sasa haziibiwi?

Nani alikuambia Africa kwa rasilimali congo ni ya kwanza na Tanzania ni ya pili? Tumia bando lako kufanya tafiti kabla ya kutoa maoni
 
Mmeachiwa muda mtatue ya nyumbani kwenu kwanza, wote wagonjwa mnakarishwaje kutibu wengine
 

Execuses tu za kushinwa kujitawala, nchi gani haina resources zenu ndio special sana? Uafrika kazi sana yani
 

Sheikh mamluki wa M23 wamekosa kazi tangu Jana, Sasa wanaotafuta wapi pa kwenda kukiwasha...!

MUNGU aepushe mbali isiwe Tanzania...!
 
Aalikwe akafanye Nini?!
 
Hayo mawazo ya hovyo sana. Yaani CCM mfanye uharamia halafu msingizie wengine. Bora mabeberu yanaheshimu haki za binadamu, CCM mnaua watu hovyo ili mbaki Mandarakani. Kama rasilimali hazina faida kwa wanachi zaidi ya CCM, zinafaida gani sasa?
 
Hawamtaki Samia
 
Mkuu vipi Kikwete anatumiwa na mabeberu kuingawa nchi?
 
Nchi za Africa zinapatanishwa na mzungu,halafu watu kutoka nchi moja ya Afrika wanalalamika au kudhihaki kua mbona wao hawakualikwa na huyo mzungu katika kuwapatanisha waafrika wenzao?

Tuna safari ndefu sana kujiondoa kwenye hizi fikra za kitumwa,

Anyway,US yeye anafaidika nini kwenye hayo mapatano? Coz hakuna kitu cha bure Dunia hii.
 
Katika geopolitics Kwa sasa hatuna ushawishi tena kikanda au kimataifa, zaidi tunahitaji kusaidiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…