Leo nimetimiza miaka 20 tangu tukio lilinishushia heshima linitokee hadi nikahama Kijiji.
Ilikuwa July 25, mwaka 2006 ambapo nilikumbwa na mkasa ambao sitoweza kuusahau.
Mara baada ya kumaliza form six nilirudi Kijijini kwetu na Kwa kipindi kile mtu aliyefika advanced Level pale Kijijini alipata kuheshimiwa sana.
Sasa diwani alianzisha ligi ya mbuzi pale Kijijini kama shukrani baada ya kushinda uchaguzi wa 2005. Katika ligi ile walihitajika waamuzi kadhaa (wa pembeni na wa kati).
Sasa, kutokana misifa, ujuaji na uchambuzi wangu uchwara wa BOLI pale Kijijini plus kuwa muhitimu wa form VI kamati ya ligi iliniamini na kunipa nafasi ya kuwa mmoja wa waamuzi.
Basi ligi ikaanza, mechi ya kwanza sikuwa miongoni mwa waamuzi. Basi tukiwa tumekaa kwenye kichuguu kilichopo pembezoni mwa uwanja, mimi nilikuwa nawakosoa vikali waamuzi waliokuwa wakichezesha, nilidiriki hata kusema, ni washamba wa soka!
Mechi iliyofuatia nikapangwa kama mwamuzi msaidizi nambari Moja (mwamuzi wa pembeni), basi kimoyomoyo nikajisema, "Leo nakwenda kuwafundisha watu vile soka huchezeshwa".
Aisee ! Mara tu ya mechi kuanza niling'amua ofside mbili tatu, kule nje makofi nilikuwa napigiwa Mimi (msomi wa Kijiji) badala ya wachezaji.
Sasa nikazidisha mbwembwe nikawa nakwenda na tukio mbiombio. Dah! Kumbe bhana mwamuzi wa pembeni huwa anatoka katikati ya uwanja hadi kwenye kona (haruhusiwi kumaliza uwanja wote) na wala Mimi sikulijua hilo.
Mimi nilikuwa natoka kutoka kona Moja kwenda kwenye kona nyingine, na nikawa najiona niko sawa tu. Nikashangaa kule nje ya uwanja watu wakawa wananisema na kunizomea, Mimi Kila nikiangalia kosa langu silioni.
Baadaye rafiki yangu mmoja akaja kuninong'oneza sababu iliyokuwa ikiwafanya watu kunizomea, dah π₯². Miguu ilikosa nguvu, hata nikaanza kutokwa na jasho mithili ya mtu aliyedinya mchana kutwa kwenye shamba la mpunga.
Baada ya timu kwenda mapumziko nilijifanya nakwenda kukojoa. Mimi huyoooo! Aise nilihama Kijiji.
Lile tukio lilinifanya mtu hata akinisifia kukereka hadi Leo, maana najua mambo huwa vipi pale mtu anayekuheshimu akikudharau. Huwa naamini ni bora zaidi mtu akikudharau halafu akuheshumu baadaye.
Anyway, miaka 20 imetimia tangu aibu ya mwaka inikumbe.
Mluga luga na sign out π