Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Makolo kwa vile mmezoea kudanganywa na chupri chupri kanji bahi unadhani kila mtu anadanganywa sio?🤣🤣🤣🤣🤣 kweli tumefikia Kila hatua kudanganywa kama watoto. Hamna lolote ni porojo tu
Amen....salute GSM na Eng HersiSALAAM ZA RAIS
Happy Birthday Young Africans Sports Club.
Leo, Februari 11, 2024 Klabu yetu kongwe na yenye mafaniko zaidi nchini Tanzania, Young Africans Sports Club imefikisha miaka 89 tangu kuanzishwa kwake.
Nichukue fursa hii kuwapongeza sana Viongozi walionitangulia, Wazee, Wanachama, mashabiki na wapenzi walioshiriki kwenye safari ndefu ya kuijenga Klabu yetu iliyoshiriki kwenye matukio mengi ya Ki- taifa ikiwemo kutafuta Uhuru wa Nchi yetu na kuijenga Tasnia ya michezo, hali inayofanya kwa sasa, Young Africans SC kuwa tunu na sio Tanzania bali Afrika kwa ujumla.
Aidha, nichukue fursa hii kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na Wanafamilia wote wa Young Africans SC kwa kumpoteza aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu yetu, Mzee Imani Madega, aliye- fariki siku ya jana.
Wakati huo huo, naungana na Watanzania wote kwenye maombolezo ya msiba wa kitaifa wa Waziri Mkuu
mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa. Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amen.
Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu wa uongozi wangu kama Rais wa Klabu hii kwa kushirikiana na Kamati yangu tendaji, tumeweza kuwa na maendeleo makubwa kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo kiutawala, kimichezo na kimiundombinu.
Leo, tukiwa kwenye sherehe za miaka 89 za kuzaliwa kwa Klabu yetu, nina Habari njema ya kuwaeleza Wanachama na Mashabiki wa Klabu yetu ya Young Africans Sports Club.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na mdhamini na mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Said Mohammed [GSM], nipende kuwataarifu Wanachama na Mashabiki wa Klabu yetu kuwa leo, GSM ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young Africans Sports Club, katika eneo la Makao Makuu ya Klabu yetu, Jangwani, Jijini Dar Es Salaam.
Nichukue fursa hii kumshukuru sana GSM kwa dhamira hiyo inayokwenda kutimiza ndoto ya Uongozi wangu, Kamati ya Utendaji na Wanachama na Mashabiki wa Young Africans kwa kuwa na uwanja wetu.
Kwa niaba ya Uongozi, Wanachama na Mashabiki wa Young Africans SC, nipende kumuahidi GSM, kuwa tutampa ushirikiano wote utakaohitajika kuhakikisha tunafanikisha ujenzi wa uwanja wetu.
Mungu ibariki Young Africans Sports Club, Mungu Ibariki Tanzania. Daima Mbele Nyuma Mwiko.
Injinia HERSI SAID, Rais wa Young Africans Sports Club
Zinduka usingizini, utajinyea serious,,, uwanja?😃Makolo kwa vile mmezoea kudanganywa na chupri chupri kanji bahi unadhani kila mtu anadanganywa sio?
Ukianza kujengwa ukuje unipige makwenzi. Nimekaa pale Fire nakusubiri!Hiyo ni hatua kubwa, muhimu na ya kuigwa.
Mo wetu kule Simba naye aige, sio kubwabwaja tu na janja janja kibao.
😂😂Jangwani hapo kwenye bwala la vyura [emoji23][emoji23][emoji23]
😂😂😂Ukianza kujengwa ukuje unipige makwenzi. Nimekaa pale Fire nakusubiri!
Na wale Wakaazi pale wamehamishwaNitaamini pale nitakapoona vifusi vimeanza kumwagwa hapo jangwani