Imetimia sasa, Yanga kuanza Ujenzi wa Uwanja wa Kisasa Jangwani

Imetimia sasa, Yanga kuanza Ujenzi wa Uwanja wa Kisasa Jangwani

Mdhamini na Mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Salim Muhammed, ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja

Kuridhia kushiriki kufanikisha ....What the Sam Hill does that mean??? Maana yake nini ?????

Mtu akijiunga maandamano ya fund raiser ya ujenzi wa bweni la wasichana tayari anakuwa ametimiza ahadi ya kushiriki kufanikisha ujenzi wa bweni la wasichana.... lijengwe, lisijengwe hayamhusu!

Mjanja mwingine huyu anawaingiza chaka Watanzania wajinga wasiojali kusoma makaratasi.....

Halafu mdhamini wa Yanga ni Ghalib mtu au Ghalim kampuni ???? Akijenga kama Ghalib mtu akashindwa kukamilisha au kutimiza vigezo au viwango wakati mshampa nusu ya haki za umiliki au umiliki 100% mkienda mahakamani kumbukeni hamuwezi kugusa mali za Ghalib kampuni.

Kingine, baada ya miaka 10 msije mkalia uwanja hauingiliki, sijui viunga vya uwanja vinajaa maji... Anaweza kupandisha juu uwanja proper, huku nje kwenye parking lot na barabara hawezi kufanya yaliyo mshinda UDART, serikali au KAJIMA. Kwa watoto wadogo, KAJIMA ni Mjapan aliyekuwa anajenga maeneo magumu in the 80s, ndio alijenga Morogoro Road kwenye mkondo wa maji Jangwani. Pameshindikana.

Dah wabongo wajuajj sana na roho ya wivu husda, vyovyote vile ni jambo la kumuunga mkono
 
Sio rahisi kihivyo labda kama anawatengenezea pitch na kuzungungusha kuta nne kama manungu kule turiani
 
Weka akiba ya maneno mkuu
Akiba ya maneno niliiweka kuanzia miaka ya 70 huko mpk Leo hamna lolote kazi ni kutaja tu uwanja utajengwa utajengwa. Tena na hivi serikali inaongeza viwanja vingine sidhani kama Simba na Yanga watajenga uwanja
 
Serikali inaangalia watu wanajenga bondeni halafu kukitokea maafa mtamlaumu Nani?

Yanga wanajenga sehem hatarishi kwa maisha ya watu.
 
sasa kama wanatoa hela kwa nini ujenzi usianze ????

na kushiriki ujenzi maana yake nini, wanatoa hela yote au kamchango kama sunah???


na sio GSM itashariki. Ni Ghalib atashiriki. Kama mtu! Kwa mujibu wa andiko la Yanga wenyewe! Anaweza kushiriki kwenye matembezi ya fund raising! Manake hawajasema atatoa hela!

Usimhukumu mleta mada ambae amebandika tangazo kama lilivyo! Soma tangazo la Yanga! Msituingize mikenge kama ilivyo kawaida.
Ndugu kama ulizoea kuingizwa mkenge huko ulikotoka basi pole sana sio huku Yanga. Sasa ngoja nikwambie kitu either by fund raising or any way Ghalib kazi yake inaweza kuwa ni kutafuta funds na kuongezea kwemye mradi. Lets assume mradi ukagharimu bilion 50 ikaja taasisi kama CRDB, NBC, PSSSF, NMB na nyinginezo wakagawana percent zao kuchangia mradi ikapatikana bilion 40 then hii 10 inayobaki ndio anaweza kuingia GSM either kwa kutoa cash au kutafuta wadhamini wake wengine by fund raising, mikopo or whatever.
 
Back
Top Bottom