Mdhamini na Mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Salim Muhammed, ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja
Kuridhia kushiriki kufanikisha ....What the Sam Hill does that mean??? Maana yake nini ?????
Mtu akijiunga maandamano ya fund raiser ya ujenzi wa bweni la wasichana tayari anakuwa ametimiza ahadi ya kushiriki kufanikisha ujenzi wa bweni la wasichana.... lijengwe, lisijengwe hayamhusu!
Mjanja mwingine huyu anawaingiza chaka Watanzania wajinga wasiojali kusoma makaratasi.....
Halafu mdhamini wa Yanga ni Ghalib mtu au Ghalim kampuni ???? Akijenga kama Ghalib mtu akashindwa kukamilisha au kutimiza vigezo au viwango wakati mshampa nusu ya haki za umiliki au umiliki 100% mkienda mahakamani kumbukeni hamuwezi kugusa mali za Ghalib kampuni.
Kingine, baada ya miaka 10 msije mkalia uwanja hauingiliki, sijui viunga vya uwanja vinajaa maji... Anaweza kupandisha juu uwanja proper, huku nje kwenye parking lot na barabara hawezi kufanya yaliyo mshinda UDART, serikali au KAJIMA. Kwa watoto wadogo, KAJIMA ni Mjapan aliyekuwa anajenga maeneo magumu in the 80s, ndio alijenga Morogoro Road kwenye mkondo wa maji Jangwani. Pameshindikana.