Imetosha Kikwete Kusemwa, Mlitaka afanyeje?

Hiyo clip uliyotaja nimeisikiliza

Haiwezi kuwa reference kwenye mada hii

Clip inaongelea kujiuzulu na sio fitina ya jk kwenye kinyanganyiro cha urais

More evidence zinahitajika ku justify claims zenu
Jk alimsaliti Sitta, anasema anataka spika mwanamke. Lakin ukimsikiliza sasahivi anajifanya kuelezea kuwa kipindi cha 1995 Sitta ndo alikuwa kiongozi wao🤔.

Kwahiyo Kwa Lowasa lazima alaumiwe. Na nadhan ndo ilikuwa wosia wa Edo. Na familia imeweza kufikisha ujumbe
 
hakika jk kasingiziwa mengi mno
 
Mkuu, kutokana na hii mada yako, hivi ni kwamba unalalamika, unashauri, unashutumu, unahitimisha, ama unaweka msisitizo? Ni haki ya kikatiba ya watu kutoa maoni yao, haijalishi kama yanakufurahisha ama la.
kutoa maoni ni sawa ila kusema uongo,kumsingizia mtu hayo sio maoni ni uchimvi
 
na huu udhaifu wa kifkra ndio unaosababisha nchi hii kuwa maskini,maana hata wasomi badala ya kujadili mambo kwa hoja wanajadili kwa uzushi
 
Kiukweli mwandishi anazo hoja. chadema walitufundisha ufisadi wa Lowasa ,tukauelewa mara ghafla kawa mgombea wao.

Chadema hili jambo limewatia kigugumizi sana .

Sasa chadema ni rafiki wa Lowasa kuliko ccm
huu ndio unaitwa unafiki
 
Sasa JK mwenyewe juzi kasema walikuwa marafiki wakubwa alafu wewe unasema hawakuwahi kuwa marafiki. Bado unataka tukuchukulie Serious kwa ulichoandika.

Ni Wajínga pekee watakaochukulia maoni yako kwa uthabiti. Hii ni kama futuhi.
ulitarajia aseme nini kilioni,aseme kuwa walikuwa maadui?
 
Naungana na mtoa hoja. Lowassa kafariki kwasababu ni lazima kila mwanadamu afariki sio kwasababu ya kuukosa Urais.

Hata kama JK angelikuwa na uwezo wa kumpitisha kuwa mgombea Urais, asingelizuia kifo chake.

Wanaomzonga JK ni wanafiki wakubwa ambao matatizo yao hawawezi kukubali kwamba chanzo ni maamuzi yao badala yake wanaamini wametengenezewa na mtu mwingine. Mtazamo huo ni dosari katika kutafuta suluhu ya matatizo kwenye jamii. Ni sawa na sisi waafrika kuwalaumu wazungu kwa kutoendelea kwetu wakati hawashiriki kwenye vikao vya maamuzi.

Lowassa alikuwa binadamu, hakuwa malaika. Ukitaka usifachafuliwe katika siasa, usifanye siasa.

Apumzike kwa amani mzee Lowassa.
 
Jmn huyu Masai aliniuma Sana kukatwa jina lake mm Niko namtumbo ila wilayanzima ilikuwa inamkubali lowasa as if alipata kuwa kijana wao

Ona sasa walio ingia badala yake
ulimkubali kwa kufata mkumbo bila kujua atakusaidia nini
 
we ni mpuuzi jk anakata jina peke yake,kwani huyo ni mkwe wa kuoa mwanae?
 
haki ya maalim seif kama kuna mtu wa kwanza kumlaumu basi ni marehemu mkapa
 
hapa unataka kuprove nini?
 
JK ni mti wenye matunda lazima upigwe mawe sana miaka mitano ya Magufuli JK katukanwa Sana bila kujali ndie aliemfanya akae hapo.Hata Lowasa angekuwa Rais bado JK angetukanwa tu Mwenyezi Mungu ampe maisha marefu JK.
Amina
 
umetumwa kuja kupoza upepo mkali unaomvumia mzee wa msoga kwa kitendo chake cha kumsulubu mwenzake kisiasa. Tuli huwezi kutuliza tufani mpaka itapita yenyewe. Unajisumbua bure, labda kama unalipwa ufanye kazi ya kutuliza upepo huu mkali
jk kakumbana na mengi na aliyadhinda yote na hata hili atalishinda tu
 
Membe na Kikwete undugu huo ulianzia wapi? Mbona hawana undugu wowote na mbaya, zaidi wamekutana miaka ya 2000s? Unajua unachoandika au kimetoka tu hapo pakunyea??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…