Pre GE2025 Imetosha! Wananchi wa Bumbuli tunakataa jina la January Makamba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mrithi wa mzee Makamba mbona wamemkataa mapema hivyo
 
Kwani Januari yeye anautaka ubunge au urais?
 
Wamechelewa sana huyu mhuni alikuwa anawatumia tu kama daraja la kutimiza ndoto yake ya kuwa Rais, hajawahi kuwa na msaada wowote kwa watu wa jimbo hilo.
 
January ni gwiji, mtoto wa mjini, ana mission na ambition zake,,,,, ! Inawezekana ni future presidential material,,,,aache kupambania ndoto zake akawapambanie nyie huko kwenye kata ? Pambaneni , hata mkimkataa chama chake kitamuweka
presidential material wa hapo sebuleni kwenu wewe na mama zako labda
jimbo lipo hivyo awe rais nchi itakuaje?eti presidential material!
kiingereza unakijua hata? unajua mana yake?
yule mvuta bangi na tambuu ndio presidential material?
 
Mleta mada naona unajitekenya na kujichekesha Mwenyewe. Kwanza wewe siyo mwana CCM. Naona unasoma upepo na kuona Mheshimiwa January Makamba anaendelea kupendwa na wananchi. na ndio maana ya kuamua kuja hapa kuanza kumchafua . Hata hivyo huwezi kufanikiwa katika lengo lako hilo.
 
Kumekucha Kumekucha Kumekucha
 
Tunaimaniiiiiiiii na Januariiiiiiiiii, oyaaa oyaaa oyaaaaaaaaa Januari kweli, kweliiiiii, kweli, kweliiiii , kweli kweli Januariiiiiii
 
January ni gwiji, mtoto wa mjini, ana mission na ambition zake,,,,, ! Inawezekana ni future presidential material,,,,aache kupambania ndoto zake akawapambanie nyie huko kwenye kata ? Pambaneni , hata mkimkataa chama chake kitamuweka
Unaweza fikiri haya ni maandiko ni ya Januari! Sawa ya kesho ni ya Mwenyezi Mungu unaweza kuishia kuyasema hayo leo lakini kesho usiyaone yakitimia.
 
Siyo swala la mleta uzi kuwa mwana CCM au la bali ni fact ambayo ipo na huwezi kushindana nayo. Ni ukweli usiopingika kuwa January hakubaliki huko kwani kwa vipindi vyote vitatu alivyokuwa mbunge alikuwa anapita bila kupingwa kwa kutumia fedha alizofisadi NSSF kuwanunua wapinzani wake wajitoe . Na pia hajafanya lolote katika Jimbo hilo wani huwa haonekani kabisa anakuja nyakati za uchaguzi tu, na jengine ni kuwa huyu alipitishwa kugombea kimagumashi kwa influence ya baba yake wa kufikia Mzee Makamba, huyu hakuzaliwa Jimboni, hakukulia Jimboni wala hajawahi kuishi Jimboni hapo hivyo hajui shida za Jimbo hilo na kuweza kuzisemea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…