Wyatt Mathewson
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 10,432
- 25,124
Ndugu zangu,
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ushauri wa JF baada ya mahojiano ya BBC umepokelewa japo hatujatangaziwa rasmi.
Kama ilivyokuwa BBC Hard talk mpango wa Tundu Lissu pia harakati zilifanywa kuomba mahojiano na Richard Quest wa CNN na Shaka Ssali wa Voa, hadi sasa habari zisizo rasmi Tundu Lissu hataenda Marekani.
Baada ya kudadisi na kautafiti nimegundua sababu ni hizi mbili lakini hazijawekwa wazi;
1.) Mapokeo hasi ya mahojiano ya BBC dhidi ya Lissu kutoka kwa watanzania
2.) Akiendelea na ziara atashindwa kujitetea dhidi ya hoja ya Spika wa Bunge kuwa amepona. Hivyo wadau wamemshauri kuwa kuendelea kuzurura kunampunguzia sababu ya kujitetea. Hii inaitwa chezea mshahara usichezee kazi.
Nitazidi kuwajuza kuhusu yatakayojiri hususani suala la maombi ya ukimbizi wa kisiasa kwa ndugu yetu Ansbert Ngurumo.
Mzee unafeli sana
Richard Quest ni mtangazaji wa biashara CNN!
Sasa Tundu Lissu yeye ni habari za kisiasa,wapi na wapi wewe mduwanzi!?
Atamuhoji amuweke kwenye kipindi gani?Kipindi cha RQ ni cha siasa?
Mbuzi wa maziwa!