Uchaguzi 2020 Imevuja: Jinsi CCM wanavyopanga kuihujumu CHADEMA

Uchaguzi 2020 Imevuja: Jinsi CCM wanavyopanga kuihujumu CHADEMA

monde arabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2017
Posts
8,781
Reaction score
13,444
Habar za muda huu ndugu wanabodi

Sote tunafahamu ya kwamba mwaka huu (2020) patakuwepo na uchaguzi hot. Habari kutoka kwenye vyanzo vya ndani zinadai kuwa CCM wamejipanga kukihujumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kufanya mambo ya aibu kama ifuatavyo;

1. Kuwanunua wagombea wa CHADEMA (hasa nafasi za Ubunge na Udiwani). Hapa mchezo utakuwa hivi; wakati kampeni zikiwa zinaendelea baadhi ya wabunge wa CHADEMA hasa wale wenye ushawishi na wanaohisiwa kushinda uchaguzi watakuwa wananunuliwa kwa fedha cash na kuahidiwa vyeo baada ya uchaguzi. Hapa mgombea wa CHADEMA akiisha kununuliwa na kuahidiwa cheo au vyeo anajitoa kwenye kinyang'anyiro cha ugombea na kuungana na CCM. CHADEMA kuweni makini sana na aina ya watu mtakaowateua kwenye nafasi tofautitofauti

2. Wagombea wa CHADEMA watakuwa wananyimwa vibali vya mikusanyiko kwa kigezo cha Corona, kutokuwepo kwa usalama na hata ikibidi watakuwa wanatumwa vijana wa CCM waliovaa sare za CHADEMA kufanya fujo na kuwakataa wagombea wa CHADEMA ili ionekane kuwa wanachama wa CHADEMA wanawakataa viongozi wao

3. CCM wanapanga kuitumia Corona virus-2019 pamoja na Ushoga kwaajili ya kuichafua CHADEMA. Hapa mchezo upo hivi;

a) CCM watawaambia Watanzania wasio na ufahamu ya kwamba "CHADEMA siyo watu wazuri, wakati Serikali inapambana na Corona wao CHADEMA walitabiri kuwa Watanzania mtakufa kama kuku" kitu ambacho siyo kweli

b) Pia, CCM watawaaminisha Watanzania kuwa CHADEMA wana-support ushoga kitu ambacho siyo kweli.

MWISHO, kataa CCM 2020 mwaga Pombe 2020 weka Tundu 2020 la kupitisha maendeleo ktk nyanja zote!
 
Ole wao wale watakaotumiwa na ccm kwa kuvalishwa nguo za chadema halafu waichafue chadema hao tushapanga kumalizana nao mara tu wanapofanya huo ujinga wao kwasababu chadema tutakuwa tunafahamiana hivo kabla ya kuja kufanya fujo waage familia zao vizuri

DUMU KUBWA
 
Hivi nyie mataga mnafeli wapi? Mtu kapandisha uzi wake kistaarabu mnaanza kumtukana matusi!

Kwani bila kutukana hauwezi kujibu kwa hoja?

Wacheni tabia za kitoto hapa janvini kama hamna hoja rudini fb mliko zoea matusi
Si ndo alivyomalizia hivyo
 
Kinachoweza kuwa mkakati wa CCM katika list yako ni kimoja tu yaani:

2. Wagombea wa Chadema watakuwa wananyimwa vibali vya mikusanyiko kwa kigezo cha Corona,kutokuwepo kwa usalama na hata ikibidi watakuwa wanatumwa vijana wa ccm waliovaa sare za Chadema kufanya fujo na kuwakataa wagombea wa Chadema ili ionekane kuwa wanachama wa Chadema wanawakataa viongozi wao

Hayo mengine yooote tumejitakia wenyewe.

1. Kuhusu kununuliwa, waanzilishi wa kununuliwa ni Mwenyekiti na Lissu walipokubali kukiuza chama kwa CCM 2015. Sasa kama Mwenyekiti na makamu wake wananunulika utawalaumu makamanda huku chini?

3. Kuhusu Corona CCM hawahitaji mkakati wowote kwa sababu watanzania wote walijionea wenyewe CHADEMA walichokuwa wanakitaka kwenye mapambano ya Corona.

4. Kuhusu Ushoga tumlaumu Lissu kutupaka matope alipokuwa anahojiwa na Steve kwenye Hard Talk.

Labda kama CCM walimtumia Lissu kukichafua CHADEMA.
 
Ccm inakubalika sana!! Imewafanyia mema sana Watanzania. Watashinda kwa kishindo.. [emoji105]
 
Ole wao wale watakaotumiwa na ccm kwa kuvalishwa nguo za chadema halafu waichafue chadema hao tushapanga kumalizana nao mara tu wanapofanya huo ujinga wao kwasababu chadema tutakuwa tunafahamiana hivo kabla ya kuja kufanya fujo waage familia zao vizuri

DUMU KUBWA
Chadema ni Chama kubwa, walijiandaa na sare wakati wa uchguzi mkuu Chadema waka badilisha sare ikala kwao.. Intelijensia ya Chadema huwezi fana nisha na upuuzi wa chama kizee
 
Kwenye suala la Corona hapo kuna shida. Viongozi walioenda kujificha badae walirudi wakachanganyikana na wale waliobaki mwisho njia hii haikuonyesha tija.
 
Kwahiyo wagombea wachadema ni wasanii tu, mpaka wanakubali kununuliwa?
 
Back
Top Bottom