Uchaguzi 2020 Imevuja: Jinsi CCM wanavyopanga kuihujumu CHADEMA

Uchaguzi 2020 Imevuja: Jinsi CCM wanavyopanga kuihujumu CHADEMA

Hivi nyie mataga mnafeli wapi? Mtu kapandisha uzi wake kistaarabu mnaanza kumtukana matusi!

Kwani bila kutukana hauwezi kujibu kwa hoja?

Wacheni tabia za kitoto hapa janvini kama hamna hoja rudini fb mliko zoea matusi Drone Camera,
Sifa kuu ya hao vijakazi ni matusi
 
Watahangaika sana ila mwisho wao hauko mbali.
Yaani kwa majivuno wanayo mpa kiongozi wao na kuona kuwa matatizo yote ya mtz, ameyamaliza nilidhania, wala hawatakuwa hata na haja ya kutumia nguvu na vihoja ili ashinde tena!!! Kwanini hawajiamini na kwa mazuri yote wanayodai wameyafanya, KISHINDOOOO CHA AWAMU YA TANO!!!
 
Kama mnajua wagombea wenu watanunuliwa ina maana chama chenu kipo kwa ajili ya maslahi binafsi na sio maslahi ya umma na pia swala la ushoga wakati tundu lissu anaojiwa na kuunga mkono ushoga hatukusikia tamko lolote toka chadema la kumkana kwamba huo sio msimamo wa chama badala yake amepewa cheo cha makamu mwenyekiti hilo tatizo mmelitengeneza wenyewe
 
Ukiwepo uchaguzi huru na wa haki pamoja haya yoooote uliyoorodhesha hapa lakini watashindwa vibaya sana.
 
1. Mbona haya ni ya kawaida tu kwenye siasa hasa katika msimu wa uchaguzi?....

2. Wanachotakiwa kufanya ni wao kutambua HILA na MBINU za adui na kuzikabili kisawasawa.....

3. Kununuliwa ni UTASHI wa mtu (mgombea), halizuiliki. Hili liko/limejificha ndani ya MOYO/NAFSI ya mtu, ni ngumu kuling'amua. Si rahisi chama kulidhibiti. Ni mtu (mgombea) aidha aamue kuuza NAFSI na UTU wake kwa vipande vya fedha watu wamdharau au ATUNZE HESHIMA NA UTU WAKE. It's a matter of making choices...

4. Cha muhimu na cha lazima ktk harakati hizi ni kufanya SCIENTIFIC SURVEILLANCE katika kambi ya adui kujua anapanga nini ili kuleta damage kwenye kambi yenu. Ukijua hayo mapema ni rahisi kuzuia na kumfyeka yeye badala yake....

5. Hili la COVID -19 na kunyimwa kibali hujaeleweka. Kibali gani wakati kibali ni Tangazo la NEC kuanza kwa kampeni rasmi kwa kila mshiriki was uchaguzi? Ungesema, watanyimwa maeneo "convenient" ya kufanyia mikutano yao ya kampeni ktk miji mingi labda Mimi ningeelewa. Hata hivyo hiyo ndiyo imekuwa hivyo ktk chaguzi zote na bado watu waliwafuata na kuwapigia kura na kushinda...!!

6. Ishu ya USHOGA na yanayofanana na hayo ni PROPAGANDA za kawaida. Muhimu ni chama kuweka watu wazuri kuipangua hoja hiyo na kisha unawapiga kwa udhaifu wao (CCM) mwingi walionao...
 
3.Ccm wanapanga kuitumia Corona virus-2019 pamoja na Ushoga kwaajili ya kuichafua Chadema.Hapa mchezo upo hivi;

a) Ccm watawaambia Watanzania wasio na ufahamu ya kwamba "Chadema siyo watu wazuri,wakati serikali inapambana na Corona wao Chadema walitabiri kuwa Watanzania mtakufa kama kuku" kitu ambacho siyo kweli

b) Pia,ccm watawaaminisha Watanzania kuwa Chadema wana-support ushoga kitu ambacho siyo kweli kwa kuwa ccm wao ndyo anao-support ushoga kwa kuliingiza Taifa kwenye mikataba yenye masharti magumu likiwemo suala la kukubaliana na ushoga ili nchi ipate misaada
Mkuu kwa haya ya nambari 3 CHADEMA kama ispojipanga itapoteza kura nyingi sana.
Ukweli ni kwamba CDM kwenye COVID-19 imefeli kama nilivyofeli mimi, niliomba lockdown angalau partial.

CDM walienda mbali zaidi na kumshambuli sana JPM , bunge na CCM juu ya hatua ilizochukua serikali kwenye kipindi kigumu cha janga hili. Hapa Magufuli kafaulu vizuri sana dara A+.

Hoja ya kutetea ushoga haitakuwa na nguvu sana wala CDM wasikose usingizi.

Haya ndiyo mawazo yangu ya kijinga na ya kufikirika tu bila tafiti.
 
Mnajitekenya na kucheka hiyo inaitwa kuweweseka,ushindi kwa CCM Ni 99%
 
Kinachoweza kuwa mkakati wa CCM katika list yako ni kimoja tu yaani:

2. Wagombea wa Chadema watakuwa wananyimwa vibali vya mikusanyiko kwa kigezo cha Corona,kutokuwepo kwa usalama na hata ikibidi watakuwa wanatumwa vijana wa ccm waliovaa sare za Chadema kufanya fujo na kuwakataa wagombea wa Chadema ili ionekane kuwa wanachama wa Chadema wanawakataa viongozi wao

Hayo mengine yooote tumejitakia wenyewe.

1. Kuhusu kununuliwa, waanzilishi wa kununuliwa ni Mwenyekiti na Lissu walipokubali kukiuza chama kwa CCM 2015. Sasa kama Mwenyekiti na makamu wake wananunulika utawalaumu makamanda huku chini?

3. Kuhusu Corona CCM hawahitaji mkakati wowote kwa sababu watanzania wote walijionea wenyewe CHADEMA walichokuwa wanakitaka kwenye mapambano ya Corona.

4. Kuhusu Ushoga tumlaumu Lissu kutupaka matope alipokuwa anahojiwa na Steve kwenye Hard Talk.

Labda kama CCM walimtumia Lissu kukichafua CHADEMA.
Thread closed
 
Mm nadhani kuhusu viongozi kuuza chama si kweli hakuna ushahidi wa hilo

Na kuhusu ushoga ungerudi kwenye katiba yetu ilioandikwa na chama chako (haki ya faragha) futeni hicho kifugu kisha ndio chadema walaumiwe

Na kuhusu korona bbc waliisha toa picha za maziko ya usiku
Na la kufanya fujo ni mkakati wa kuleta fujo ili uchaguzi uahirishwe
 
Back
Top Bottom