Habar za muda huu ndugu wanabodi
Sote tunafahamu ya kwamba mwaka huu (2020) patakuwepo na uchaguzi hot. Habari kutoka kwenye vyanzo vya ndani zinadai kuwa CCM wamejipanga kukihujumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kufanya mambo ya aibu kama ifuatavyo;
1. Kuwanunua wagombea wa CHADEMA (hasa nafasi za Ubunge na Udiwani). Hapa mchezo utakuwa hivi; wakati kampeni zikiwa zinaendelea baadhi ya wabunge wa CHADEMA hasa wale wenye ushawishi na wanaohisiwa kushinda uchaguzi watakuwa wananunuliwa kwa fedha cash na kuahidiwa vyeo baada ya uchaguzi. Hapa mgombea wa CHADEMA akiisha kununuliwa na kuahidiwa cheo au vyeo anajitoa kwenye kinyang'anyiro cha ugombea na kuungana na CCM. CHADEMA kuweni makini sana na aina ya watu mtakaowateua kwenye nafasi tofautitofauti
2. Wagombea wa CHADEMA watakuwa wananyimwa vibali vya mikusanyiko kwa kigezo cha Corona, kutokuwepo kwa usalama na hata ikibidi watakuwa wanatumwa vijana wa CCM waliovaa sare za CHADEMA kufanya fujo na kuwakataa wagombea wa CHADEMA ili ionekane kuwa wanachama wa CHADEMA wanawakataa viongozi wao
3. CCM wanapanga kuitumia Corona virus-2019 pamoja na Ushoga kwaajili ya kuichafua CHADEMA. Hapa mchezo upo hivi;
a) CCM watawaambia Watanzania wasio na ufahamu ya kwamba "CHADEMA siyo watu wazuri, wakati Serikali inapambana na Corona wao CHADEMA walitabiri kuwa Watanzania mtakufa kama kuku" kitu ambacho siyo kweli
b) Pia, CCM watawaaminisha Watanzania kuwa CHADEMA wana-support ushoga kitu ambacho siyo kweli.
MWISHO, kataa CCM 2020 mwaga Pombe 2020 weka Tundu 2020 la kupitisha maendeleo ktk nyanja zote!
LOOoo, mkuu, hizi ni hujuma, au ni mchezo wa 'kindergaten'!
Sioni hujuma yoyote hapo.
CHADEMA wakishindwa kukabili hizi unazoziita 'hujuma' basi hawajawa tayari kukabidhiwa nchi, na hawastahiri kamwe kumlalamikia yeyote.
Hujuma kama za kuzuia magazeti yasitangaze habari za vyama vya upinzani, naona hii umeisahau...; hii nayo ni hujuma inayowashinda wapinzani kuikabili?
Kawastue CCM, kama hizo ndizo hujuma walizopanga, watafanikiwa tu kama wapinzani wataruhusu ujinga huo
Ukiniambia hujuma, kama za kuwaweka ndani viongozi wote wa upinzani wakati wa kampeni hadi uchaguzi, hapo nitaanza kukusikiliza kwa umakini mkubwa.
CCM wakianza kutumia dola kuwavuruga na kuwapiga wapinzani, nitakusikiliza, na pengine kuanza kuchangia mawazo ya kujikinga zidi ya hujuma kama hizo.
Hao vijana wa CCM wasiotambulika kwa vile tu wamejivika magwanda ya CHADEMA, wao hawana nyama na damu? Hakuna hata mmoja CHADEMA wasioweza kuwatambua kwamba hao sio vijana wao?
Huko CHADEMA hakuna vijana?
Mkuu, mada yako ni nyepesi mno. Hukutumia muda vizuri kuibuni. Nenda kajaribu tena.