Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo Wote!
1. Mimi nimesoma Dini Kupitia Ukristo, dhehebu Usabato.
2. Ninauelewa kiasi WA mambo ya Dini nafikiri katika mambo ninayoyajua akilini mwangu ukiacha Mahusiano, saikoloji, sosholoji ma Falsafa basi Dini ni moja ya mambo ninayoyajua kwa kiwango cha kuridhisha kwa vijana wa umri wangu.
3. Binafsi siongozwi na Dini, ingawaje yapo mambo mengi nimejifunza kupitia Dini. Kwangu Dini ni Kama shule ya Maadili hivi.
4. Kitabu cha Biblia na Quran kwangu sio vitabu vitakatifu kama wengi wanavyovichukulia. Kwangu ni vitabu vya kifalsafa ambavyo Watibeli tunaweza kuvisapoti maeneo yenye logic na kuvikosoa maeneo tunayoyaona hayajakaa sawa.
5. Wakati nakua, nikiwa napewa masomo ya biblia, masomo ya unabii kupitia vitabu na lesson za wasabato. Nilikuwa mbishi Sana hasa pale ninapoona dini na dhehebu jingine linapingwa kwenye mijadala ya lessson nikiwa na Wazazi na Walezi wangu.
6. Sikupenda kwa sababu niliona haiko sawa. Kusema Waislam dini zingine sio sahihi wakati kwa uelewa wangu wakati ule niliona pia kwenye dini niliyopo kuna mapungufu nilikuwa nakataa nakiwapinga wakubwa wangu. Nikitoa mifano kupitia concepts na matendo ya waumini.
7. Hali hiyo ilileta ubishi na kukaripiwa mara kwa mara. So ubishi na kusakamwa hata humu mtandaoni ni Jambo ambalo Nina uzoefu nalo tangu nikiwa mtoto.
8. Kila kabila linajiona bora kuliko kabila jingine. Wakati nakua wazazi na walezi wangu walikuwa wakiponda Makabila mengine. Wakitaja sifa mbaya. Sasa Mimi nikisikia hivyo nakataa kwa kutoa mifano ya watu waliondani ya kabila letu wenye tabia hizo mbaya.
Kiufupi nilikuwa wale opposer yaani mpingaji hasa nikiona unaongea uongo.
9. Baadaye niligundua ni tabia waliyonayo watu wengi. Kila mwamba Ngoma huvutia kwake. Huku wakiponda wengine.
10. Hapo ndio Wazo la Utibeli lilipoingia. HAKI, UKWELI, UPENDO na AKILI.
11. Kwamba kukubali Ukweli hata kama unakuumiza. Kufikiri, kuchunguza kabla ya kuamini.
12. Mimi ni Mtibeli. Ninaamini katika Falsafa za Ukristo kuliko Uislam na uyahudi.
Ndio maana kwenye Utibeli kuna nguzo ya UPENDO.
13. Uislam na Uyahudi havijajengwa kwenye msingi mkuu wa upendo. Ni Dini Ambazo msingi wake Mkuu ni Sheria, haki na hukumu.
14. Kinachonishangaza ni kwamba licha ya falsafa ya ukristo ya Upendo inakuwaje Siku za hivi Karibuni kumekuwa na dhihaka na kejeli kwa walee wanaoamini katika Uislam na Quran.
15. Kama Mtibeli najua ni Kweli asilimia 90% Uislam ume-copy kwenye Uyahudi na Ukristo. Kisha kumi ndio Muhammad na tamaduni za kiarabu.
16. Pamoja na hivyo lakini sioni sababu ya watu kuwashambulia Waislam na uislam.
17. Humu JF, nenda Facebook, Nenda Instagram utakuta pages na account nyingi zikishambulia ma kukejeli uislam na waislam.
18. Nikajua ni bongo, nilipofuatilia nikagundua kumbe ni suala la ulimwengu karibu wote. Ulaya, America, Asia, na Afrika.
19. Hakuna sababu ya kuchukiana kwa vile watu wanavyoamini au wanavyoamua kuamini.
20. Msingi mkuu wa maadili ni kujiheshimi na kuheshimu wengine. Kujipenda na kupenda wengine.
Kuwa na mipaka. Huo ndio msingi mkuu wa dini zote.
21. Kujifunza uislam ili kuongeza maarifa sio tatizo. Kuamua kuamini uislam pia sio tatizo.
Kama ilivyo kwa kujifunza ukristo, ubudha, uhindu, uyahudi ili kuongeza maarifa sio tatizo na hata ukiamua kuamini.
22. Muhimu kuliko ni kutomlazimisha mtu aamini kile unachoamini. Au kulazimishwa kuamini kile ambacho hutaki kuamini.
23. Kama Mtibeli, tunapojadili mijadala ya kidini tunajadili kama watu wenye ufahamu kwa kutumia mantiki sio kwa kama waumini.
Hii iwe kwako
Kijakazi na wenzako.
Usifikirie dini kisiasa.
Kuweni kama Wahindu au Wayahudi. Au Watibeli.
Nimemaliza
TaikonMaster
Kwa sasa, Bunju, DSM