#COVID19 IMF: Tanzania lazima iweke wazi takwimu za COVID-19 ili ipate msaada wa dharura

#COVID19 IMF: Tanzania lazima iweke wazi takwimu za COVID-19 ili ipate msaada wa dharura

Mimi naona tuwape takwimu ya bupiji ngapi na fukiza plus ngapi na malimau, tangawizi,pilipili kichaa na vitunguu vilivyotumika mpaka sasa na gharama za kujenga mashine ya nyungu ndio watupatie kama msaada, ni vihela vichache tu hamna haja ya kukopeshana, au nasema uongo ndugu zangu ? [emoji205][emoji2223][emoji1787]
Bupiji nilikuwa nimeisahau aisee..

Bongo hii bhana!!!
 
Bupiji nilikuwa nimeisahau aisee..

Bongo hii bhana!!!
Wabongo hatujambo katika kuchangamkia fursa, hii ya tiba asili tulivunja rekodi ya kuwa nchi ya kwanza duniani yenye dawa nyingi za corona kuliko idadi ya wagonjwa wenyewe 🤣
 
Katika miaka mitano Magufuli kakopa sh. 31 Trillion,japo alikuwa hazungumzii kukopa.
Ni pesa nyingi mno,Tatizo alikopa kwenye mabenki yenye riba kubwa lakini hayako tiyari kutufutia madeni hasa kwa wakati mgumu wa Covid-19.
 
Ukikubali kuolewa sharti ulale bila chupi!!!!!!. Sisi tuna Elimu lkn hatuna akili. Madini, gesi maziwa utalii lkn bado sisi ni omba omba. W.H.O hawawezi kumvimbia kifua china kwa sababu china hatembezi bakuli.

Tuolewe mara ngapi?
 
Yaani pesa haifiki hata tilioni 1.5 na tunavyojidai nchi Ina rasilimali za kutosha, kwa nini tusiikatae? Au bado sisi ni masikini? Uchumi wa Kati vipi?
 
Yaani pesa haifiki hata tilioni 1.5 na tunavyojidai nchi Ina rasilimali za kutosha, kwa nini tusiikatae? Au bado sisi ni masikini? Uchumi wa Kati vipi?
Aisee umeongea kitu cha maana sana. Hiyo pesa si makusanyo yetu ya mwezi tu. Tunahangaika nayo ya nni?
 
Kwanini takwimu hizi zinafanywa siri?

Kwamba zinafanywa siri ni kutotutendea haki sisi wenyewe kama waathirika nambari 1 wala hata si kwa sababu ya incentive yoyote.
Hazipo hizo takwimu, tufanyeje sasa, tutunge feki au?
 
Yaani pesa haifiki hata tilioni 1.5 na tunavyojidai nchi Ina rasilimali za kutosha, kwa nini tusiikatae? Au bado sisi ni masikini? Uchumi wa Kati vipi?
Hiyo ni almost 1Trilion.

Kuingiza trilion 1 kwenye uchumi faida zake ni nyingi sana kuliko kuleta kiburi kuikataa.
 
Huyu mama kayataka mwenyewe haya sasa watamwambia aweke kwanza lock down ndo wampe hela. Mama kusanya kodi achana na hao we unaona mwenzako alikupuka ama vipi
 
Back
Top Bottom