IMF yaidhinisha ufadhili wa Dola Milioni 900 kwa Tanzania kwa ajili ya Bajeti na kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya Hewa

Kila siku mikopo lakini nafuu ya maisha kitaa hakuna, ina faida kwa nani sasa?!.
 
Ndio Nchi kupigwa Mnada?
Haipigwi mnada ila utaona sehemu muhimu kuchukuliwa na mabeberu tukishindwa kulipa mikop. Maana kuna nchi zimewahi chukulia viwanja vyao vya ndege kisa mikopo isiyolipika na masharti lukuki.

Lakini pia mkuu kwenye hali ya kawaida hebu angalia tunavyokopa hovyo mfano SGR ni mikopo mingapi umesikia imekopwa kwa mradu huo tu ,viongozi wanapiga sana hela kwa jambo linaloitwa mikopo na sisi tunaona sawa
 
Kila siku mikopo lakini nafuu ya maisha kutaa hakuna, ina faida kwa nani sasa?!.
Toka lini mikopo lukuki inayotumiwa vibaya ikaleta nafuu ya maisha mkuu...hebu nenda kakope hela halafu kanywee pombe kisha utaona maisha yako yatakavyokua mabaya jama ya digi digi ndo kinachotokea kwetu serikali ina matumizi mabaya ya hela halafu tunaumia sisi kwa kodi za ajabu.
 
Kama mabio alihusika kuleta chura kwa wapigakura basi na alaaniwe yeye na vizazi vyake
 
Hizi habari za kukopa tutaacha lini ndugu zangu wapendwa Watanzania?
 
Huyo chura ndio nani?
Yupo kwenye taasisi ya urais ameshasema yanayofanyika yote kwenye urais wake sio yeye ni taasisi ndio inaamua kwa hio msijemkaanza kumlaumu yeye ilaumuni taasisi sio yeye yeye hausiki
 
Chadema watadhani wamepewa ruhusa ya kula mayai ya kuchemsha na maharage ili waanze kupitisha upepo, kwa kuwa wameona kuna hela za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa
 
Nazihurumia hizo hela
 
Ngoja wakope ili wataalam wa kutumbua nchi waendelee na projects zao, its nonstop hadi maza aachie madaraka as nchi iko autopilot. Sidhani kama kuna eneo halina upigaji kipindi hiki.

It's a real shame kuwa na utawala wa namna hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…