IMF yaidhinisha ufadhili wa Dola Milioni 900 kwa Tanzania kwa ajili ya Bajeti na kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya Hewa

IMF yaidhinisha ufadhili wa Dola Milioni 900 kwa Tanzania kwa ajili ya Bajeti na kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya Hewa

Lini wataanza kugawa hizo pesa na sisi tuzione mfukoni
 
Nisaidie tafsiri ya neno financing kwa kiswahili. Kwa mfano tukisema the world bank is financing the construction of 320km road from Chalinze to Kibaigwa.
Ni kutoa pesa,je wanatoa kwa misingi gani,mkopo au ufadhili?!..ulishasikia aliyekua mfadhili wa yanga gulamali kaidai yanga?!..au Azim dewji kuidai Simba?
 
Saizi mnakula tu, siku wakitaka mzigo mnatoa macho.
 
Ni kutoa pesa,je wanatoa kwa misingi gani,mkopo au ufadhili?!..ulishasikia aliyekua mfadhili wa yanga gulamali kaidai yanga?!..au Azim dewji kuidai Simba?
Mkuu Mo anafadhili simba, anadai ama hadai?😂

Anyway, hiyo ndio dhana ya neno financing ama ufadhili.
 
Bodi ya Wakurugenzi ya IMF imeidhinisha Mkopo kiasi Cha $900 Milioni sawa na karibu Shilingi Trilioni 2.4 Kwa Tanzania Ili kuisaidia kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Hali ya hewa kwenye uchumi.

Aidha ieleweke kwamba Serikali inakopo kile ambacho kimeidhinishwa kwenye Bajeti,haifangi kiholela.

Aidha ieleweke kwamba Nchi inakopeshwa Kwa sababu Ina uwezo wa kulipa kulingana na uimara wa Uchumi wake. Sio Kila Nchi inapewa Mkopo.

My Take: Katika kipindi hiki Nchi inatekeleza miradi mikubwa ya Maendeleo, Tuendelee kukopa kwani mikopo inaharakisha maendeleo hususani Miradi ya kimkakati

==============


Shirika la kimataifa la fedha (IMF) Alhamisi limesema bodi yake ya utendaji imeidhinisha ufadhili wa dola milioni 786.2 kwa Tanzania kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Shirika hilo la kifedha linakamilisha pia tathmini tofauti ya kuruhusu malipo ya dola milioni 149.4 kwa ajili ya msaada wa bajeti.

Mamlaka za Tanzania zina dhamira ya kuendelea kutekeleza mageuzi ya kudhibiti uthabiti wa kifedha, kuimarisha ufufuaji wa uchumi, kukuza ukuaji endelevu na shirikishi, IMF ilisema katika taarifa.

Katika miaka mitatu iliyopita, utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan ulifanya mageuzi mbalimbali ya kiuchumi kwa lengo la kurudisha ukuaji wa uchumi katika kiwango cha ukuaji wa pato la taifa la kabla ya janga la Covid wa asilimia 6 hadi asilimia 7.

Mpango wa mageuzi ya uchumi wa Tanzania bado umeendelea kuwa imara, IMF imesema, na kuongeza kuwa ukuaji wa uchumi uliongezeka mwaka 2023 baada ya kupungua mwaka 2022.

Uchumi wa Tanzania ambao unategemea utali, madini, kilimo na viwanda, umeendelea kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa yanayochochewa na kuongezeka kwa sekta ya huduma, kulingana na Benki ya Dunia.

Uchumi wa Tanzania unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka huu, kutoka asilimia 5.1, waziri wa mipango na uwekezaji katika Ofisi ya Rais, Kitila Mkumbo alisema wiki iliyopita.

DW Kiswahili

PIA, SOMA:
Hizi ndio hela za rushwa kwa vigogo IMF hua wanatoa. Eti mamilioni kwa ajili ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mwananchi gani ataweza kuona au kujua hizo hela zimefanya kazi ya faida yoyote kwake? Wanatoa sifa za bure tu huku wenyewe wananchi tunajua ni ulaji rushwa na ubadhilifu serikali hii imejaai. Magufuli alipokua anawaomba mikopo kwa reri au bwawa la nyerere walimnyima maana wanajua ni mambo ya maendeleo ya kweli ila hivi viinimacho wanatolea hela za kuliwa na huku wakikamilisha biashara ya kukopesha yenye faida kwao. Wanajua kuna mashirika yao yatakuja kushirikiana na vigogo kula hela zitakazobakia deni kwa nchi bila manufaa ila kuweka deni tu kwa wananchi.
 
inabidi tununue hizi gari nyingi ili kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa

2021_Toyota_Land_Cruiser_300_3.4_ZX_(Colombia)_front_view_02.png
 
Nimebubujikwa na machozi😭😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom