IMF yaidhinisha ufadhili wa Dola Milioni 900 kwa Tanzania kwa ajili ya Bajeti na kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya Hewa

Lini wataanza kugawa hizo pesa na sisi tuzione mfukoni
 
Nisaidie tafsiri ya neno financing kwa kiswahili. Kwa mfano tukisema the world bank is financing the construction of 320km road from Chalinze to Kibaigwa.
Ni kutoa pesa,je wanatoa kwa misingi gani,mkopo au ufadhili?!..ulishasikia aliyekua mfadhili wa yanga gulamali kaidai yanga?!..au Azim dewji kuidai Simba?
 
Saizi mnakula tu, siku wakitaka mzigo mnatoa macho.
 
Ni kutoa pesa,je wanatoa kwa misingi gani,mkopo au ufadhili?!..ulishasikia aliyekua mfadhili wa yanga gulamali kaidai yanga?!..au Azim dewji kuidai Simba?
Mkuu Mo anafadhili simba, anadai ama hadai?😂

Anyway, hiyo ndio dhana ya neno financing ama ufadhili.
 
Hizi ndio hela za rushwa kwa vigogo IMF hua wanatoa. Eti mamilioni kwa ajili ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mwananchi gani ataweza kuona au kujua hizo hela zimefanya kazi ya faida yoyote kwake? Wanatoa sifa za bure tu huku wenyewe wananchi tunajua ni ulaji rushwa na ubadhilifu serikali hii imejaai. Magufuli alipokua anawaomba mikopo kwa reri au bwawa la nyerere walimnyima maana wanajua ni mambo ya maendeleo ya kweli ila hivi viinimacho wanatolea hela za kuliwa na huku wakikamilisha biashara ya kukopesha yenye faida kwao. Wanajua kuna mashirika yao yatakuja kushirikiana na vigogo kula hela zitakazobakia deni kwa nchi bila manufaa ila kuweka deni tu kwa wananchi.
 
inabidi tununue hizi gari nyingi ili kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa

 
Nimebubujikwa na machozi😭😭😭😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…