Ina maana hizi Bodaboda wanazigawa bure kama peremende?

Ina maana hizi Bodaboda wanazigawa bure kama peremende?

Kiukweli ccm imeshindwa Kuendesha nchi Yaani miaka 60 ya uhuru nchi bado maskini hii inatuma sana

Sasa tumepata uhuru wa nini full ufisadi na uwizi wa fedha za umma

Huku mnatia taifa kwenye Madeni yasiyolipika

Wewe unasemaje haikuumi hii kitu?
Mnaolalamika mnataka vijana wafanyiwe nn kama elimu zao chenga , kulima hawataki , na kuajiri wote kwa mkupuo serikali haiwezi na kuwaondoa wwfanyakazi waliopo ili iingize wapya haiwezi pia ,mnatukana CCM mnataka chama gani kiingie , au huu utopolo wa akina Mbowe na zitto ??? Mtakuwa na makamasi kwenye ubongo
 
Kiwanda cha vilema....Ruangwa basi sawaa....tusubiri muda taongea
 
Mnaolalamika mnataka vijana wafanyiwe nn kama elimu zao chenga , kulima hawataki , na kuajiri wote kwa mkupuo serikali haiwezi na kuwaondoa wwfanyakazi waliopo ili iingize wapya haiwezi pia ,mnatukana CCM mnataka chama gani kiingie , au huu utopolo wa akina Mbowe na zitto ??? Mtakuwa na makamasi kwenye ubongo
Kama Kuna bodi ya mikopo inayotoa mikopo Kila mwaka kwa wanafunzi wa elimu ya juu maelfu kwa maelfu, na wanahitimu na kukosa ajira, huoni huo ndo uzwazwa ambao unaisababishia serikali hasara?? Wangeajiriwa si wangeilipa serikali na wengine wangenufaika??
 
Si ameshasikia hakuna kupita bila kupingwa. Kwanza ameshatumikia miaka 10 ya Uwaziri Mkuu , angepumzika awaachie wengine

Yeye ni nani mpaka we Waziri Mkuu miaka kwa zaidi ya miaka 10?

Kwangu mimi katika Mawaziri Wakuu waliowahi kuongoza Tanzania huyu ni wa mwisho.
Nafikiri hawezi kugombea tena ubunge.
Huwezi kutoka kuwa waziri mkuu urudi kuwa mbunge wa kawaida.
 
Kila mara anagawa bodaboda sasa ni nani atapanda ya mwenzie, hivi hamna chochote anachoweza kuwafanyia mbadala ya bodaboda![emoji848]
 
Nafikiri hawezi kugombea tena ubunge.
Huwezi kutoka kuwa waziri mkuu urudi kuwa mbunge wa kawaida.
Hizo pikipiki anagawa target yake ni nini, ni Ubunge, na kama Ubunge anafikiria kuendelea na Uwaziri Mkuu
 
Sasa ndugu unafikiri hizo pikipiki anagawa target yake ni nini, ni Ubunge, na kama Ubunge anafikiria kuendelea na Uwaziri Mkuu
Atakuwa hajielewi.
Hawezi kuendelea kuwa waziri Mkuu awamu yake inaishia 2025 akifanikiwa kumaliza.
Kuwa mbunge baada ya kustaafu uwaziri mkuu nao ni ujinga.
Ukishafikia nafasi za juu hupaswi kuja kurudia nafasi za chini.

Ona ndugai hawezi tena kuwa mbunge baada ya awanu hii kukamilika.
 
Ni kweli kabisa, labda ajipange huko mbeleni baadae sana baada ya miaka 15 agombee kuingia nafasi namba 1.
 
Ili tuendelee twahitaji mambo manne yaliyo ya muhimu, kwanza watu, pili ardhi, Siasa safi na uongozi Bora. Siku hizi imeongezeka na bodaboda, katika standard za kimataifa, bodaboda haijawahi kuwemo, hata maendeleo ya Ulaya yalianza na ardhi, baadae wakawa na human resource Bora kabisa inayofanya ubunifu.

Bodaboda ni hand to mouth economy
 
Ni kweli kabisa, labda ajipange huko mbeleni baadae sana baada ya miaka 15 agombee kuingia nafasi namba 1.
Ni ngumu sana Kasimu kuwa namba moja.
Ambao wangeweza kumbeba wanawaza watoto wao wawe namba 1
 
Ni ngumu sana Kasimu kuwa namba moja.
Ambao wangeweza kumbeba wanawaza watoto wao wawe namba 1
Ila ukweli uwezo hakuna kabisa, hata huo Uwaziri Mkuu basi tu. Anyway ameingia kwenye rekodi ya Mawaziri wakuu wachache kuhudumu miaka 10, kama sikosei ni wawili tu

Marais wawili aliohudumu chini yao walikaribia kumtoa kwenye nafasi ya Uwazi Mkuu
 
Bado safari ni ndefu mkuu kumaliza ni Majaaliwa ya Mungu kama jina lake
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi pikipiki 100 zenye thamani ya sh. milioni 260 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili wazitumie kufanya biashara ya usafirishaji.

Akizungumza na vijana wa Ruangwa kwenye hafla ya kukabidhi pikipiki hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya CWT, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, Waziri Mkuu alisema utoaji wa pikipiki hizo ni muendelezo wa mpango wa ofisi ya Mbunge wa kuwawezesha vijana, wanaume, wanawake na wazee.

"Mwaka 2016/2017 tulichukua pikipiki 235 na kuzigawa kwenye wilaya yote hii. Na jambo zuri kwa sasa, kwenye Serikali ya awamu ya sita, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Tanzania na yeye ameamua kuwa na kada ya wasafirishaji wa wadogo, wa kati na wakubwa.”

View attachment 2573910
Chanzo: Mwanahabari
Huyo anayeshake naye mkono ni kijana?
 
Ili tuendelee twahitaji mambo manne yaliyo ya muhimu, kwanza ardhi, pili watu, Siasa safi na uongozi Bora. Siku hizi imeongezeka na bodaboda, katika standard za kimataifa, bodaboda haijawahi kuwemo, hata maendeleo ya Ulaya yalianza na ardhi, baadae wakawa na human resource Bora kabisa inayofanya ubunifu.

Bodaboda ni hand to mouth economy
Siasa safi Tanzania haziwezi kuwepo hadi wafuatao wasiwepo nchi hii:
Jk
Kinana
Makamba sr
Hawa ni virusi...walitakalo huwa
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi pikipiki 100 zenye thamani ya sh. milioni 260 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili wazitumie kufanya biashara ya usafirishaji.

Akizungumza na vijana wa Ruangwa kwenye hafla ya kukabidhi pikipiki hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya CWT, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, Waziri Mkuu alisema utoaji wa pikipiki hizo ni muendelezo wa mpango wa ofisi ya Mbunge wa kuwawezesha vijana, wanaume, wanawake na wazee.

"Mwaka 2016/2017 tulichukua pikipiki 235 na kuzigawa kwenye wilaya yote hii. Na jambo zuri kwa sasa, kwenye Serikali ya awamu ya sita, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Tanzania na yeye ameamua kuwa na kada ya wasafirishaji wa wadogo, wa kati na wakubwa.”

View attachment 2573910
Chanzo: Mwanahabari
NDIO watakaokimbiza masanduku ya kura mwaka 2030
 
Kila mara anagawa bodaboda sasa ni nani atapanda ya mwenzie, hivi hamna chochote anachoweza kuwafanyia mbadala ya bodaboda![emoji848]

Wakati tayari mkoa wa Lindi pamoja na wilaya ya Ruangwa wanasema : source : UZINDUZI RASMI WA MUONGOZO WA UWEKEZAJI MKOA WA LINDI
ESRF na uongozi wa Mkoa wameafikiana uzinduzi rasmi ufanyike siku ya tarehe 27 Novemba, 2019

2. Vipaumbele vya uwekezaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni ambavyo ni:-

  • Uwekezaji unaolenga kukuza utalii kupitia fursa zilizopo za misitu/asili na fukwe,
  • Usindikaji wa korosho katika kuongeza thamani,
  • Vyuo vya ufundi stadi na ujuzi,
  • Viwanda vya kusindika mafuta ya kula,
  • Usindikaji wa mhogo,
  • Upandaji bustani za miche ya matunda,
  • Upasuaji mbao,
  • Vifaa vya ujenzi,
  • Uchimbaji na usindikaji wa madini,
  • Usindikaji wa mazao ya mboga na matunda,
  • Ufugaji wa nyuki na usindikaji wa mazao yake hususani asali
  • Viwanda vya maji ya kunywa/chupa
  • Kilimo cha umwagiliaji wa kibiashara hususani Mpunga na mbogamboga
  • Ufugaji wa samaki na viumbe wengine wa baharini.
3. Sababu kumi na moja za kuwekeza katika mkoa wa Lindi zinabainishwa kuwa ni:-

  • Hali ya utangamano kisiasa na ulinzi wa uhakika na matukio machache ya uhalifu,
  • Uwingi wa mali asili ambazo zinatoa fursa kwa mapana katika kuongeza mnyororo wa thamani.
  • Uwepo wa ardhi ya kutosha na inayofaa kwa kilimo cha msimu, umwagiliaji, misitu na maendeleo ya viwanda.
  • Uwekezaji mkubwa wa miaka ya karibuni kwa miradi mikubwa katika maeneo jirani hususani Kiwanda cha Cement cha Dangote, uchimbaji wa gesi asilia na viwanda vinavyotarajiwa vya mbolea na uchimbaji wa madini ya Kinywe n.k.
  • Msukumo wa Serikali katika kuanzisha kituo maalumu cha uwekezaji (Special Economic Zone (SEZ) and a business park) karibu na eneo la uwekezaji wa kuchakata gesi asilia la Kikwetu.
  • Ukuaji wa soko la ndani ya mkoa- Kwa sasa mkoa unao wakazi wapatao 1, 082,346 kulinganisha na wakazi 787,624 waliokuwepo wakati wa Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2002 na wakazi 864,652 waliokuwepo wakati wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
  • Kuimarika kwa miundombinu muhimu katika kukuza uchumi ikiwemo kukamilika kwa barabara ya lami kutoka Dar Es Salaam hadi Mtwara. Barabara inayopitia Lindi –Masasi na Mtambaswala katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji; ukarabati na upanuzi wa bandari ya Mtwara, kukamilika kwa bomba la usafirishaji mafuta kutoka Mtwara hadi Dar Es Salaa pamoja na ukarabati wa miundombinu ya kusambazia umeme.
  • Mipango madhubuti iliyopo ya kimkakati ya kupanua bandari ya Lindi pamoja na ujenzi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa- Sokoine.
  • Vivutio vya asili vya utalii ikiwemo fukwe ambazo hazijachafuliwa, Mabaki ya magofu ya kale na mapango ya Kilwa, Hifadhi ya Selous n.k
  • Uwepo wa taasisi zisizokuwa za Kiserikali katika kuchochea maendeleo kuanzia za kimataifa na zile za ndani ya nchi.
  • Utashi wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii miongoni mwa Uongozi wa mkoa na Halmashauri katika kusaidia uanzishaji biashara mkoani, wakati Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) likiwa na dhamira ya dhati katika kukuza uchumi wa ndani miongoni mwa wakazi wa Lindi.
“ Hautajutia kuamua kuwekeza katika mkoa wa Lindi
 
Back
Top Bottom