Ni kwa ajili ya kuiridhisha nafasi yake!
1. Katika majina anayoyatumia kwa sasa, jina la katikati na la mwisho yote ni ya baba yake
2. Japo jina la kwanza ambalo ndilo lake ni zuri, anataka abaki nalo lakini litanguliwe na jina lake lingine jipya alilojichagulia mwenyewe ukubwani. Kwa mfano, kama alikuwa akiitwa JOSEPH TREKTA JUMA ambapo Trekta na Juma ni majina ya baba yake (Trekta lilikuwa jina la utani la baba yake na Juma ndilo jina halisi la baba yake), majina yake mapya yatakuwa JAMES JOSEPH JUMA ambapo JAMES na JOSEPH ni majina yake (la James amejipa mwenyewe ukubwani) na Juma ni la baba yake, kwa hiyo jina la babu/ukoo wake halitatumika kwenye utambulisho wake
3. Ili kuwemo na mfanano wa majina yake na ya watoto wake. Watoto wake wanatumia majina 2: JOSEPH JUMA kama majina ya ubin. Kwa mfano, mwanawe wa kiume, tumpe jina la ALMASI, anaitwa ALMASI JOSEPH JUMA.
NB. Majina yote hapo juu ni ya kutungwa lakini yanaakisi hitaji la mwenye hitaji tajwa hapo juu.