Wafunge na wakitaka waue wapinzani wote nchini!
Wafunge na wakitaka waue wana-CCM wote wanaoonekana kuupinga utawala nchini!
Wafunge, na wakitaka waue wanaharakati wote nchini wanaopinga haya yanayotokea!
Wafunge, na wakitaka waue wakosoaji wote nchini wanaoipinga serikali!
Wakifanya hivyo, hapana shaka taifa litabaki na misukule ya CCM peke yake ni ile misukule inayototea utawala kwa kuangalia ukabila na ukanda! Lakini hata hiyo misukule, ipo siku na yenyewe itakuja tu kuaguliwa na akina Dr. Manyaunyau, na badala ya kuendelea kulishwa unga kama chakula chao, hapo itaanza kudai ugali uliopikwa, na ndipo utatimia ule msemo kwamba, hapana serikali ya kidhalimu iliyopata kudumu milele duniani!!! Udhalimu usipoisha muongo huu, haidhuru hata kama utaisha karne ijayo! Na wala haigopeshi ikiwa wapinga udhalimu wote wataingia kaburini kabla hata mambo hayajatengemaa, kwani hawa watakuwa ndio mashahidi siku ya hukumu!