Tetesi: Inadaiwa Bernard Membe atakuja kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi

Tetesi: Inadaiwa Bernard Membe atakuja kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi

mtzmweusi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
8,658
Reaction score
8,994
Habari wakuu,

Anaandika kada wa CCM, Bolleni Ngeti

Uoga ukikuzidi unaweza kujikuta unajikimbia. Mchakato wa kumfungulia kesi ya utakatishaji wa Fedha (Money Laundering), Bernard Membe kuhusu kesi mfu ya MEIS ya kiwanda cha saruji mkoani Lindi umeiva.

Habari nilizozipata ni kwamba hiyo ndiyo silaha ya mwisho kumzuia Membe asigombee Urais kupitia CCM. Wadadisi wa mambo wananiambia uamuzi huu unaweza kumaanisha usemi wa Niguse Ninuke.

68489673_187808778887258_6930633385178038272_n.jpg
 
Membe atagombea Urais wa TZ kupitia ACT-Wazalendo.

Hii ni mbinu ya kuzigawa kura kutoka kambi ya upinzani.

Makosa yaliyofanyika kwa Lowassa hayawezi kufanyika tena ambapo kunakuwa mgombea mmoja pekee mwenye nguvu kutoka upinzani.

Wakati CDM wameamua Lissu awe mgombea wao, CCM lazima wazigawe kura zake.

Watu wanacheza ngoma za CCM bila kujua!

Siasa ni sayansi na sio uanaharakati na ushabiki!
 
Wapinzani watasiamamisha mgombea mmoja
Membe atakwenda kuchuana humohumo ndani ya CCM
 
Wafunge na wakitaka waue wapinzani wote nchini!

Wafunge na wakitaka waue wana-CCM wote wanaoonekana kuupinga utawala nchini!

Wafunge, na wakitaka waue wanaharakati wote nchini wanaopinga haya yanayotokea!

Wafunge, na wakitaka waue wakosoaji wote nchini wanaoipinga serikali!

Wakifanya hivyo, hapana shaka taifa litabaki na misukule ya CCM peke yake ni ile misukule inayototea utawala kwa kuangalia ukabila na ukanda! Lakini hata hiyo misukule, ipo siku na yenyewe itakuja tu kuaguliwa na akina Dr. Manyaunyau, na badala ya kuendelea kulishwa unga kama chakula chao, hapo itaanza kudai ugali uliopikwa, na ndipo utatimia ule msemo kwamba, hapana serikali ya kidhalimu iliyopata kudumu milele duniani!!! Udhalimu usipoisha muongo huu, haidhuru hata kama utaisha karne ijayo! Na wala haigopeshi ikiwa wapinga udhalimu wote wataingia kaburini kabla hata mambo hayajatengemaa, kwani hawa watakuwa ndio mashahidi siku ya hukumu!
 
😢😢😢

Back
Top Bottom