Tetesi: Inadaiwa Bernard Membe atakuja kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi

Tetesi: Inadaiwa Bernard Membe atakuja kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi

Sheria za nchi ni msumeno hukata pande zote. Bugirichato naye kahujumu uchumi na kuna ushahidi wa kutosha tu kuhusu hili wakiwemo Mkapa, Kikwete na wengi wengineo.

Wote wapandishwe kizimbani bila upendeleo wowote ule na kukomoana kwa kutumia madaraka vibaya.

Kama alihujumu kweli ni haki yake ya msingi akishtakiwa.
 
Kama anafanya kazi nzuri na anadhani anakubalika sasa wasiwasi wa nini si atateuliwa tena kugombea?
Aache demokrasia ndani ya chama ifanye kazi yake!
Je Membe ni msafi kiasi kwamba kila kinachomuhusu inaonekana ni siasa?
 
Ngoja tuone...

Ukizungumza kuhushu uhujumi uchumi, karibia asilimi 99.9 ya viongozi wote walishawahi kufanya ubathilifu, na wengine bado wanaendelea kufanya...


Angali Report zote za CAG... Hakuna kiongozi msafi karibia wote machoni kama watu, mioyoni hawana tu,,,



Cc: mahondaw
 
Hakuna anayemuogopa Membe, kama kweli wanajiandaa kumfungulia kesi basi angalau mahakama itasaidia kumuondoa kwenye hizi tetesi na kuwa huru iwapo ni msafi, kama ni kweli alikwapua basi jela ni yetu sote!
kesi anayofunguliwa itamalizika hadi magu amalize muda wake. sasa hapo huwo usafi unaoutaka wewe utadhibitishwaje?
 
Jamaa mwoga balaa!

Mbona anafanya vyema tu hofu ya nini.?

Fuatilia hata historia yake kwenye ubunge, kama alishinda kihalali basi ni mara moja tena mwanzoni, hajawahi tena kushinda bila fugisu. Anafanya vizuri upande wa miundombinu tu, huko kwingine anajua fika watu wakipata jukwaa la kuongea watabadili mitazamo. Urais ni zaidi ya miundombinu. Kwa ujumla sio mshindani ndio maana hataki ushindani wa aina yoyote.
 
UWOGA WA WANINI KM ANAKUBALIKA?

Kwa taarifa yako haogopi chochote kwakuwa ana madaraka, isipokuwa anajua fika hakubaliki kwa kiwango cha kushinda, hivyo inabidi atumie madaraka yake kuhakikisha udhaifu wa yeye kutokuweza ushindani unaondoka.
 
Kama alihujumu Uchumi,acha sheria ichukue mkondo wake.

Na ww ajuza kwa kushabikia uovu hujachacha. Ni kweli alihujumu uchumi hilo halina ubishi, lakini kipi kilifanya awamu hii ya tano ifunge mahakama ya mafisadi kwa kisingizio kwamba haina wateja? au Membe alizaliwa na kuanza ufisadi baada ya ile mahakama kufungwa? Kwetu sisi hizo ni siasa chafu.
 
Membe atagombea Urais wa TZ kupitia ACT-Wazalendo.

Hii ni mbinu ya kuzigawa kura kutoka kambi ya upinzani.

Makosa yaliyofanyika kwa Lowassa hayawezi kufanyika tena ambapo kunakuwa mgombea mmoja pekee mwenye nguvu kutoka upinzani.

Wakati CDM wameamua Lissu awe mgombea wao, CCM lazima wazigawe kura zake.

Watu wanacheza ngoma za CCM bila kujua!

Siasa ni sayansi na sio uanaharakati na ushabiki!
Hili sio picha la maigizo kama unavyo waza wewe hii ni serious inshu kuwa membe anataka madaraka. [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Na huyo aliyekwapua nyumba za Serikali na kununua kivuko uozo kwa 8 bilioni sheria haistahili kuchukua mkondo wake!? 😳
Hii ni kuhusu Membe. Kila jambo na wakati wake. Awe mwingine amekwapua nyumba hiyo haimfanyi Membe kutoface sharia kama kweli alihujumu uchumi.
 
Nimekuambia umeshazeeka ngozi ya uso imekubana, hakuna mtu anashoboka na jizee. Mpelekee Polepole ndio anavutiwa na mijizee.
Kwani shida ipo wapi yakhe. Kuzeeka ni neema jamani. Wangapi wamekufa bila kufikia uzee. Tena nakushukuru sana kwa kunitamkia hii neema. Maneno yanaumba. Namuomba Mungu anipe neema ya kufikia uzee nione wajukuu zangu na wajukuu zao. Hapa hoja ni Membe na siyo uzee wangu.
Mbona unatoka nje ya topic ?
 
Hii habari ya kufungwa kwa Membe nitaipokea kwa roho moja, maana ilikuja nafasi ya katiba mpya, yeye na Makada wenzake wa ccm ikiwepo hawa wanaowafanyizia sasa wakavuruga na kuhujumu zoezi lile, sasa hivi acha waone madhara ya madaraka ya rais ndio akili zitawakaa vizuri. Funga huyo muhuni hata kifungo cha maisha ajue hujuma na siasa za hila hazilipi.
 
Wafunge na wakitaka waue wapinzani wote nchini!

Wafunge na wakitaka waue wana-CCM wote wanaoonekana kuupinga utawala nchini!

Wafunge, na wakitaka waue wanaharakati wote nchini wanaopinga haya yanayotokea!

Wafunge, na wakitaka waue wakosoaji wote nchini wanaoipinga serikali!

Wakifanya hivyo, hapana shaka taifa litabaki na misukule ya CCM peke yake ni ile misukule inayototea utawala kwa kuangalia ukabila na ukanda! Lakini hata hiyo misukule, ipo siku na yenyewe itakuja tu kuaguliwa na akina Dr. Manyaunyau, na badala ya kuendelea kulishwa unga kama chakula chao, hapo itaanza kudai ugali uliopikwa, na ndipo utatimia ule msemo kwamba, hapana serikali ya kidhalimu iliyopata kudumu milele duniani!!! Udhalimu usipoisha muongo huu, haidhuru hata kama utaisha karne ijayo! Na wala haigopeshi ikiwa wapinga udhalimu wote wataingia kaburini kabla hata mambo hayajatengemaa, kwani hawa watakuwa ndio mashahidi siku ya hukumu!
ujumbe murua
 
Kwani shida ipo wapi yakhe. Kuzeeka ni neema jamani. Wangapi wamekufa bila kufikia uzee. Tena nakushukuru sana kwa kunitamkia hii neema. Maneno yanaumba. Namuomba Mungu anipe neema ya kufikia uzee nione wajukuu zangu na wajukuu zao. Hapa hoja ni Membe na siyo uzee wangu.
Mbona unatoka nje ya topic ?

Ufikie uzee mara ngapi? Mada ni Membe kweli, ila nimekuambia kwa uzee wako sio wa kushabikia dhuluma.
 
Back
Top Bottom