Inadaiwa huyu ndiye Moses Lijenge (luhende)

Inadaiwa huyu ndiye Moses Lijenge (luhende)

Hawa jamaa ni wanajeshi wastaafu na walikuwa mtaani wanaendesha maisha yao. Mbowe alikuwa anatafuta walinzi/body guards ndiyo kuna jamaa (naye mwana jeshi) akawainganisha na Mbowe. Kilichofuata hawa jamaa wakadakwa mwaka jana na mwaka huu Mbowe akaiunganishwa nao.
mbowe nae.kwani walinzi binafsi hakuwaona
 
Hawa jamaa ni wanajeshi wastaafu na walikuwa mtaani wanaendesha maisha yao. Mbowe alikuwa anatafuta walinzi/body guards ndiyo kuna jamaa (naye mwana jeshi) akawainganisha na Mbowe. Kilichofuata hawa jamaa wakadakwa mwaka jana na mwaka huu Mbowe akaiunganishwa nao.
Asante mkuu,umenifungua.....Mbona kama Bado wadogo walistaafu kwa mujibu wa Sheria au walifukuzwa?
 
Walitoka congo operation ikasemekana Wana battle confusion ,,yan matatzo ya akili ndo wakaachishwa kazi ila wote ni makomandoo
Komandoo gani anapigwa na mahita Hadi anajinyea?
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Ikitokea hukumu ikala kwa pt sijui wazee wa bakabaka watachukua hatua gani, tusubiri mahakama ifanye kazi yake Kwanza maana ni ukakasi mtupu
 
Komandoo gani anapigwa na mahita Hadi anajinyea?
Unajielewa kwel wewe kwan komandoo ni jiwe? Hata CDf akipigwa analia komandoo ni prefesional tu na technique kwan ulidhan ni nn?
 
Inasikitisha sana ukiifatilia hiyo kesi huyo mke wa Adamoo kapata tabu sana ukisikiliza ushahidi wake unaweza kutoa machozi...
 
Kuna Yule Mkuu Wa Kituo Cha Chamwino Mpaka Kesho Kimya Ndugu Zake Wanahaha Police Inajibu Mtoro Kazini
Naona hapa ilifutwa nataman kujua nini kiliendelea! Gazet la mwananchi nao sikuhiz kimya
 
Nimeona picha ikizunguka mtandaoni watu wanaomba wamuone mahakamani naye apandishwe kizimbani.

Narudia tena: INADAIWA kuwa ndiye yeye.

View attachment 1955929

Utata umeibuka alipo mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya kufadhili ugaidi inayomhusisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, aitwaye Moses Lijenge kama yuko hai au amefariki dunia.

Utata huo umeibuliwa leo Jumanne Septemba 28, 2021 na shahidi wa pili wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, Mohamed Ling'wenya wakati akihojiwa na mawakili .

Shahidi huyo ambaye ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo anatoa ushahidi kwa lengo la kujiridhisha uhalali wa utoaji wa maelezo ya mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa ambayo mawakili wa utetezi walipinga yasipokewe mahakamani kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashtaka wakidai yalichukuliwa nje ya muda wa kisheria na mshtakiwa huyo alitoa maelezo hayo baada ya kuteswa na kutishiwa.

Awali, shahidi wa kwanza katika kesi ya msingi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai aliieleza mahakama kuwa wakati wakiwakamata watuhumiwa wawili huko Moshi, mtuhumiwa wa tatu Lijenge hawakumpat, licha ya kumtafuta sehemu mbalimbali, hivyo wakaamua kuwapeleka Dar es Salaam watuhumiwa hao wawili.

Lakini katika ushahidi wake wa msingi jana, shahidi huyo alidai wakati wakitolewa kituo cha polisi kwenda Mbweni mmoja wa maaskari alimweleza kuwa mwenzake Moses Lijenge wameshamtupa kwa sababu alijidai kuwakimbia.

Alipohojiwa na wakili wa Mbowe, Peter Kibatala leo Jumanne shahidi huyo amedai alivyoelezwa na askari yule kuwa mwenzao Lijenge wameshamtupa alielewa kuwa ameshauawa.

Akihojiwa zaidi na Kibatala, Mohamed amedai hajawahi kumsikia akitajwa mahali popote na upande wa mashtaka kama Lijenge ataunganishwa katika kesi hiyo, hivyo hajui kwa hakika kama yuko hai au ameshafariki.

Kwa sasa shahidi huyo wa pili upande wa utetezi katika kesi ndogo anaendelea kuhojiwa na upande wa mashtaka kuhusiana na ushahidi wake.

Chanzo: Mwananchi 28. 09. 2021
Mama Tanzania ndio hii

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Lakini na chifu naye kwa nini alikubali kuingizwa mkenge hivyo!
 
Back
Top Bottom