Inadaiwa kuwa serikali ya Tanzania imeishiwa pesa na kuongeza wasiwasi wa kukamilika kwa SGR huku kukiwa na ahadi za uongo

Mi naona wangepiga miradi hii kwa awamu, wangeishia tu phase 1 ya Dar- Makutupora.wangeacha mradi ufanye kazi miaka kadhaa,wafanye tathimini,wajipange phase 2 kwenda Tabora kisha Phase3 kwenda Mwanza.
Kitu kingine cha muhimu si kila kiongozi anaweza kuhimili ujenzi wa miradi hii mikubwa. (MAMA HAWEZI KAZI).
Bora hata yule Paolo angekuwa Rais .
 
Kama rasalimali siyo mali, basi nchi kama Botswana isingeendelea! Una mawazo mafinyu sana, na unashindwa kuangalia dunia inakwendaje iwapo refernce yako yote ni kwenye ujenzi wa Tazara.
Naona hujaelewa maana ya "rasilimali sio mali", Rasimali ni potential tu, kama maji ya mto, usipojenga bwana na kuweka mitambo huo umeme utausikia tu kwa majirani zako.

Botswana wamebadilisha rasilimali kuwa mali, ndio maana unawatolea mfano hapa. DRC wanaongoza kwa Rasilimali na hawana chochote.
 
Mwenye miradi yake kafa nayo ndio trend yetu waafrika, hata kwenye biashara za wabantu mitaani ni ivyo ivyo kwa kiasi kikubwa mwanzilishi akifa anaowaachia mali sio muda mrefu wanapoteza kila kitu.

Hapo bado fines za kuchelewesha mradi na malipo ya wakandarasi jumlisha inflation. Kama JNHPP waliikuta imebakiza miezi michache iishe wakaunga kwa miaka mitatu nakusingizia waliikuta bado sana, ni kwa miujiza tu watamaliza hiyo reli.

Kumbuka ‘bi-tozo’ kakopa ndani ya miaka mitatu kushinda maraisi wote walivyokopa katika muda wao hata wale wa miaka 10 kawapita kwa ukopaji wake kwa kipindi kifupi.

Hakuna namna gęsi itagaiwa sawa na bure soon ‘economic hit men’ washafanya yao. Kuchekea mafisadi hakujawahi endeleza nchi yeyote duniani.
 
Absolutely mkuu, hayo yote lazima wakandarasi wata claim in near future
 
Pesa zipo, miaka hii miwili ina vipaumbele vyake. Kumbuka sisi hatufanyi kwa ajiri ya wajao, tunafanya kila kitu kwa manufaa yetu.
 
CCM NI JANGA LA KITAIFA
 
hata hazina huko kuna malipo mengi tu yamekwamba ninavyosikia. wenye wake zenu wafanyakazi wa umma tuambieni kama ni kweli.
 
Hii miradi yote inatekelezeka iwapo tu wizi na rushwa vingedhibitiwa
Ni kweli kabisa mkuu......hakuna commitment ya kutosha halafu fedha zinakuwa zinabadilishiwa matumizi sababu za kisiasa na kuacha miradi ya kimkakati.
 
Pesa zipo, miaka hii miwili ina vipaumbele vyake. Kumbuka sisi hatufanyi kwa ajiri ya wajao, tunafanya kila kitu kwa manufaa yetu.
Kwa hio hao Watoto mnaozaa mnategemea wataendesha vipi Uchumi kama nmajiangalia ninyi pekee?
 
Jk aliishi angani zaidi kuliko Tanzania nchi ikafilisika.

Bado napiga hesabu nione kama Chief Hangaya naye Kama anaikaribia rekodi ya Jk
 
Mngewatangazia Watanganyika wajue. Waache kulalamika miradi inasimama kumbe sio kipaombele kwa sasa.
 
Mkuu weka bayana ushahidi wa ubadhirifu, wizi na upondwaji wa hela hizo za mkopo. Tuhuma zako bila udhibitisho ni upotoshaji ulio kubuhu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…