Inadaiwa Mwanamke ana wastani wa mawazo 70,000 kwa siku

Inadaiwa Mwanamke ana wastani wa mawazo 70,000 kwa siku

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Uzi tayari.

Ila mimi sikubaliani na utafiti kwamba eti wanawake hawana Kinga ya kutosha kutokana na kuwaza zaidi.

Kama hawana Kinga mbona wanaishi Umri mrefu kuliko wanaume?

======

Imeelezwa kuwa mwanamke ana wastani wa mawazo 70,000 kwa siku na inaaminika asilimia 70 huwaza vitu vya kufikirika au hasi jambo linalowafanya wengi kutozalisha kinga mwili za kutosha.

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa mwanamke ana wastani wa mawazo 70,000 kwa siku na inaaminika asilimia 70 huwaza vitu vya kufikirika au hasi jambo linalowafanya wengi kutozalisha kinga mwili za kutosha.

Hivyo kutokana na maumbile yake, anashauriwa kuacha kushindana na mwanaume kwa kuwa hujiongezea msongo wa mawazo na hivyo kuwa hatarini kupata mshtuko wa moyo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Machi 11, 2022 na mbobezi wa magonjwa ya moyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi wakati akitoa mada katika mdahalo wa wanasheria wanawake uliyofanyika katika mtandao wa Zoom kuhusu mradi wa Mwanamke Imara unaotekelezwa katika mikoa mitatu.

“Unapoweka mashindano unajiweka hatarini kiafya, kila kitu unachokifanya leo kuanzia chakula unachokula, aina ya mazoezi unayoyachagua, namna unavyolala, msongo wa mawazo na unapokosa muda wa kupumzika haya yote yanaathiri kesho yako na afya yako baadaye,” amesema.

Profesa Janabi amesema hivyo ni miongoni mwa vihatarishi vinavyomfanya mwanamke awe katika hatari zaidi ya kupata kiharusi kuliko mwanaume.

Mradi wa Mwanamke Imara una lengo la kutokomeza aina zote za ukatili wa kijinsia unaotekelezwa kwenye mikoa hiyo na mashirika manne ambayo ni Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA), WILDAF, KWIECO na TANLAP Kwa ufadhili wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).
 
Uzi tayari.

Ila mimi sikubaliani na utafiti kwamba eti wanawake hawana Kinga ya kutosha kutokana na kuwaza zaidi.

Kama hawana Kinga mbona wanaishi Umri mrefu kuliko wanaume?

View attachment 2148995
Ni kwasababu wanapataga rutuba toka kwa wanaume, imagine nourishments zilizoko kwenye ule mzigo ME anapopiga bao [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Uzi tayari.

Ila mimi sikubaliani na utafiti kwamba eti wanawake hawana Kinga ya kutosha kutokana na kuwaza zaidi.

Kama hawana Kinga mbona wanaishi Umri mrefu kuliko wanaume?

View attachment 2148995
Tungemuomba atupe hilo chapisho tujiridhishe kama mbinu iliyotumika katika utafiti huo inaweza kuwa na mantiki ya hitimisho hilo.

Hiyo ni taarifa kubwa,hasa ukichukulia kwamba inatolewa mwezi wa siku ya mwanamke duniani
na anayetoa taarifa ni mtu mhimu kwenye tasnia ya afya.
 
Back
Top Bottom