Inadaiwa Picha maarufu ya Ronaldo na Messi ilikuwa edited bila wao kukutana, kutokuwa marafiki ndio chanzo kikuu

Inadaiwa Picha maarufu ya Ronaldo na Messi ilikuwa edited bila wao kukutana, kutokuwa marafiki ndio chanzo kikuu

Kama hivi au siyo
1669029236107.jpg
 
Hilo yai vipi mbona lina likes nyingi limefanyaje, au ndo ile yai na kuku kipi kilianza, basi wangemweka na kuku tuje moja
 

Ni picha iliyojizolea umaarufu mkubwa watu wengi wakidhani picha hio ilikuwa ni ya kweli na ilipigwa kwa lengo la kumbukumbu, Stori ipo tofauti kabisa.

Picha hii imeandaliwa kwajili ya mikakati ya kutangaza na kuifanyia promoshen kampuni kubwa ya nguo "luis vutton", kampuni hii iliingia mkataba na wachezaji hawa na kuwalipa pesa ndefu ili wawe kwenye picha moja.

Wawili hao walikubali mkataba huo ila kwenye kupiga picha hawakuweza kupiga pamoja kirahisi, ilibidi Messi aende kwa muda wake na baada ya kuondoka akaja Ronaldo nae akapiga kivyake, baada ya hapo wataalam wa photoshop ndio wakaziunganisha.

Kwa makubaliano ya mkataba iliwabidi wote waposti kwa pamoja picha hio kwenye mitandao yao ya kijamii.

Hivyo si kama watu wengi wanavyodhani kwamba picha iliyopigwa ilikuwa wapo pamoja ama walipiga kishkaji iwe kumbukumbu kwao.

Kutokuwa na mazoea ndio chanzo kikuu
Ikumbukwe Ronaldo hakumpigia kura Messi kwenye Balon D' Or ya mwaka juzi.

Wawili hao hakuna aliye mfollow mwenzake kwenye mitandao ya kijamii
Kwa hiyo ww uliamini hiyo ni picha halisi?
 
Sio maadui na wala sio marafiki.

Imetrend kwa sababu hao jamaa ni watu maarufu zaidi kwenye ulimwengu wa mpira.
Na ni nadra kupata picha wakiwa pamoja.
 
Sasa kwann limetrend hvyo,ebu na wew jaribu kusimamisha yai
Tunaishi katika dunia ambayo ujinga au mambo ya kijinga ndio yanayopata umaarufu na heshima kubwa katika jamii, wakati mambo ya maana na umuhimu yakipewa hadhi ya chini na kupuuzwa
 
Back
Top Bottom