Yaani sadaka zote hizo na waumini mamilioni alafu wanaomba msaada kwa serikali ya CCM?
Hii ni fedheha kubwa sana.
View attachment 3550046
Hapana sio fedheha, kuna vitu vinahitaji pesa ndefu sana kuliko hata makusanyo ya sadaka ya nchi nzima.
Hili hutokea kwa viongozi wa dini zote, hata ukisikia Mufti ametibiwa nje ya nchi, fedha za Waislamu wote Tanzania hazitoshi kumhudumia hivyo huwa ni serikali huwa inaokoa jahazi.
Tena afadhali ya Wakristo, ni sadaka zinaendesha TEC!, na viongozi wetu wote tunawatibia kwa fedha zetu, na wana bima kubwa za afya, lakini amini usiamini, michango ya Waislamu wa Tanzania, sio tuu haiwezi hata kuendesha Bakwata!, bali hata kumuwekea tuu Mufti bima ya afya hawawezi!, Mufti akiugua hata kutibiwa tuu hospital za ndani, ni serikali ndie inamtibu
BAKWATA Ina matatizo ya Uendeshaji. Je, itaziweza Mahakama za Kadhi?!
Zile AC zote pale makao makuu ya Bakwata, ikiwemo ac ya ofisi ya Mufti zimefungwa kwa ufadhili wa taasisi fulani ya Kikristu!, na baada ya kufungiwa ac, siku mfadhili amepita pale kusalimia, akukuta ac zote japo zipo, zimezimwa!, akauliza kulikoni ac zipo haziwashwi, akaambiwa zinakula sana umeme wa luku, hivyo wameamua wasiziwashe!. Ufadhili akakubali atakuwa analipa bili yote ya umeme ya Bakwata kuwasha ac!, Waislamu wangejua kuwa hata umeme wa Bakwata unalipwa na taasisi ya Kikristu, ingekuwa ni aibu kiasi gani?, uzuri wa taasisi hiyo ni low profile haisemi wala haitambi!. Niliwahi kushauri humu
Waislamu mliofanikiwa kwa Elimu ya Shule za Mission badala ya Madrasa kuweni na Shukrani kwa Wakristo waliowafikisha hapo mlipo
P