Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Naamini katika nguvu ya Mungu ya uponyaji kupitia maombi, lakini Mwamposa hapana, sio mtumishi wa kweli wa Yesu Kristo!
 
Lakini Mwamposa siyo Nabii, ni Mtume.
 
Basi maadam ni mtu mzima,achaneni naye.
 
Mwamposa anasadaka yake inaitwa SADAKA YA KUJIMALIZA hiyo sandakan unatoa pesa yote uliyokuwa nayo mpka nauli yaan akikisha umejimaliza kweli [emoji1][emoji1][emoji1]baada ya hapo utaanza kuona miujiza
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],Wajinga ndio waliwao.
 
Wanaponywa magonjwa Gani? Au ndo Yale Yale magonjwa yasiyoonekana Kwa macho? Maana ndio gear ya hawa matapeli. Mara kisukari, pumu, uvimbe and so on!!
Siamini kama watu wote wale wanapangwa.
Hivi kwani haiwezekani watu kupona Magonjwa?
Kama tunamuamini Mungu,basi tuamini pia kuwa anaponya.
 
Sio Mimi peke angu maelfu elfu wanao jazana kawe wameshuhudia matendo makuu ya MUNGU...

Mkuu kama upo dar es salaam siku Moja nenda pale nenda na ajenda yako...
Fuata formula za pale utakuja hapa kutoa mrejesho...
Kumbe kuna kufuata formula tena sasa kuna tofauti gani ni mganga wa kienyeji?
 

Mwamposa ana akili kaona muda wake unakaribia kuisha kajenga hoteli na kuanza kulima parachichi. Kawaacha wasiojua mbele Wala nyuma wanamsindikiza. Ngoja aendelee kuwaibia tu mpaka muelewe.
 
Nilikuaga kama wewe siku Moja tena nilikua kama Kiranga
Mimi nilikua mfano wa sauli roho ngumu sana....
Ikafika siku nikakata shauri miaka Sasa the rest is history...

Hongera kwa kukata shauri, umefanya uamuzi mzuri Sana.
 
Nilikuwa nasikiliza wimbo wa joseph nyuki tegemeo langu. Anasema yesu anaponya magonjwa yote kisukari, ukimwi, saratani, n.k. Cha ajabu jamaa ni kiwete, hana mkono. Sasa najiuliza hilo la kumrudishia mkono yesu kashindwa ama vipi?

Alikuwa na mkono ukakatwa. So sio natural ulemavu.
 
Ila najua amebakia tu kuwapeleka msitu wa Shakahola🤸🤸🤸
 
Sio Mimi peke angu maelfu elfu wanao jazana kawe wameshuhudia matendo makuu ya MUNGU...

Mkuu kama upo dar es salaam siku Moja nenda pale nenda na ajenda yako...
Fuata formula za pale utakuja hapa kutoa mrejesho...

Acheni propaganda. Maelfu gani unaongelea?. Yule akija Dodoma watoa ushuhuda wanakuwa watu wa shinyanga na akienda Tabora watoa ushuhuda wa musoma na kahama. Sio wa hapo hapo. Tuache kutumika na shetani hukumu yake ni mbaya Sana.
 

Mwamposa Tangu auwe watu Moshi namuona zaidi ya scam Tena mbaya Sana.
 
Kuna wagonjwa pia huwa wanapona wakati anafundisha pasi na kutumia hayo maji na mafuta.

Hizo ni PR stunts. Siku moja mfuatilie Nabii mmoja anajiita Kanyari kule Kenya alivyodakwa ndio utaelewa utapeli unavyofanywa. Aliaanda kundi la watu kutoa ushuhuda. Mwamposa damu za Moshi zinamlilia, na Wala hakutoa pole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…