Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Rekodi ya Yesu mbona ilishavunjwa siku nyingi tu

Sio sababu watumishi wa sasa wako vizuri kuliko Yesu la .Ila Yesu Mwenyewe aliomba na kuwaombea watakaofuata baadaye wavunje hiyo rekodi kwa maombi yake

Enzi za Yesu alihubiria watu wachache tu kwa sauti yake tu sasa hivi spika zipo xaweza wafikia wengi kuliko mkutano wa Yesu pia kipindi cha Yesu aliweza wafikia tu waliohudhuria mkutano wake tena wa lugha yake tu bila mkalimani leo watu waweza hubiria dunia nzima mabilioni ya watu kupitia television, nk wa mataifa na lugha mbalimbali kupitia Television ,YouTube, nk kwa kutumia wakalimani nk

Kufanya wanaomwamini makubwa kuliko yeye ni majibu ya maombi aliyoomba sio sababu mtumishi yuko smart sana.Hata wewe waweza fanya makubwa kuliko Yesu

Yohana 14:12​

Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Naamini katika nguvu ya Mungu ya uponyaji kupitia maombi, lakini Mwamposa hapana, sio mtumishi wa kweli wa Yesu Kristo!
 
Dada angu wewe rahis kuibiwa ,hayo Ni maigizo, na wanaandaliwa kabisa ,wanapewa script kabisa


Manabii wote unaowona hapa Tz Ni matapeli

Hivi unaelewa Cheo Cha UNABII lakini?

Nabii Ni daraja Kati ya Mungu na mwanadamu

Nabii kifupi anaongea na Mungu ,nabii anaweza kukutajia hata ufanye Nini ili usife , Rejea nabii Isaya kwa mfalme hezekia

Sasa mwamposa alileta balaa kule Moshi watu wakafa. ..wengine wakajeruhiwa ,akawakimbia

Kwanini asiwamwagie Mafuta na maji wapone na waliokufa wafufuke , zaidi akakimbia na akalindwa na serikali
Lakini Mwamposa siyo Nabii, ni Mtume.
 
Sikio la kufa halisikii dawa hakuna wa kumzuia kwenda kwenye ibada za Mwamposa maana yeye sio mtoto mdogo ni mtu mzima na ana shughuli zake na mji wake, yeye anaamini siku moja atapona kupitia Mwamposa Ila hakuna hata dalili za kupona hali ipo vile vile
Basi maadam ni mtu mzima,achaneni naye.
 
Mwamposa anasadaka yake inaitwa SADAKA YA KUJIMALIZA hiyo sandakan unatoa pesa yote uliyokuwa nayo mpka nauli yaan akikisha umejimaliza kweli [emoji1][emoji1][emoji1]baada ya hapo utaanza kuona miujiza
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],Wajinga ndio waliwao.
 
Wanaponywa magonjwa Gani? Au ndo Yale Yale magonjwa yasiyoonekana Kwa macho? Maana ndio gear ya hawa matapeli. Mara kisukari, pumu, uvimbe and so on!!
Siamini kama watu wote wale wanapangwa.
Hivi kwani haiwezekani watu kupona Magonjwa?
Kama tunamuamini Mungu,basi tuamini pia kuwa anaponya.
 
Sio Mimi peke angu maelfu elfu wanao jazana kawe wameshuhudia matendo makuu ya MUNGU...

Mkuu kama upo dar es salaam siku Moja nenda pale nenda na ajenda yako...
Fuata formula za pale utakuja hapa kutoa mrejesho...
Kumbe kuna kufuata formula tena sasa kuna tofauti gani ni mganga wa kienyeji?
 
Kuna principal mkuu may be hukuzifuata na muda sijaenda pale ila ukiitaji.....
Twende pale pamoja tutakuja shuhudia hapa....

Alaf usidhani wanao enda pale hawana akili timamu MWAMPOSA kasaidia sana watu...

Kuna matendo makuu ya MUNGU nimeshuhudia....na wengi wameya shuhudia ..

Mwamposa ana akili kaona muda wake unakaribia kuisha kajenga hoteli na kuanza kulima parachichi. Kawaacha wasiojua mbele Wala nyuma wanamsindikiza. Ngoja aendelee kuwaibia tu mpaka muelewe.
 
Nilikuaga kama wewe siku Moja tena nilikua kama Kiranga
Mimi nilikua mfano wa sauli roho ngumu sana....
Ikafika siku nikakata shauri miaka Sasa the rest is history...

Hongera kwa kukata shauri, umefanya uamuzi mzuri Sana.
 
Nilikuwa nasikiliza wimbo wa joseph nyuki tegemeo langu. Anasema yesu anaponya magonjwa yote kisukari, ukimwi, saratani, n.k. Cha ajabu jamaa ni kiwete, hana mkono. Sasa najiuliza hilo la kumrudishia mkono yesu kashindwa ama vipi?

Alikuwa na mkono ukakatwa. So sio natural ulemavu.
 
Nimebahatika kuona vipindi kadhaa vya mchungaji Mwamposa.

Yawezekana ukimtoa Yesu (Kwenye ukristo) kiumbe mwenye kufanya miujiza mingi hapa duniani anaweza kuwa huyu Mchungaji.

Sitaki kuhukumu kama ni mkweli au Lah, ila kwa wanaoshuhudia kwenye vipindi vyake anaweza vunja rekodi.

Nadhani ile miujiza ya Yesu ya uponyaji huyu mchungaji ataivunja rekodi zake, isipokuwa Kulisha watu 5000 ambao walikula na kusaza na kufufuka kwa yesu.

Kuna yoyote amepatwa na muujiza wa Mwamposa haswa uponyaji humu?
Ila najua amebakia tu kuwapeleka msitu wa Shakahola🤸🤸🤸
 
Sio Mimi peke angu maelfu elfu wanao jazana kawe wameshuhudia matendo makuu ya MUNGU...

Mkuu kama upo dar es salaam siku Moja nenda pale nenda na ajenda yako...
Fuata formula za pale utakuja hapa kutoa mrejesho...

Acheni propaganda. Maelfu gani unaongelea?. Yule akija Dodoma watoa ushuhuda wanakuwa watu wa shinyanga na akienda Tabora watoa ushuhuda wa musoma na kahama. Sio wa hapo hapo. Tuache kutumika na shetani hukumu yake ni mbaya Sana.
 
Samahani,
Huwa sipendi kuweka maisha yangu in public Kwa sababu zangu binafsi ambazo sio nzurii kuzielezea hapa......

Nacho weza kusema Kwa Sasa kama MWAMPOSA ni SCAM hawezi kuwapanga watu wote wale Kuna maelfu na maelfu ya watu Mungu kawatendea kupitia madhabahu ya Arise & Shine...

Cha kukushaur kama itakupendeza jarib kwenda pale na ajenda yako yeyote...

Najua utakuja kutupa ushuhuda hapa juu ya Matendo makuu ya MUNGU 😊

Mwamposa Tangu auwe watu Moshi namuona zaidi ya scam Tena mbaya Sana.
 
Kuna wagonjwa pia huwa wanapona wakati anafundisha pasi na kutumia hayo maji na mafuta.

Hizo ni PR stunts. Siku moja mfuatilie Nabii mmoja anajiita Kanyari kule Kenya alivyodakwa ndio utaelewa utapeli unavyofanywa. Aliaanda kundi la watu kutoa ushuhuda. Mwamposa damu za Moshi zinamlilia, na Wala hakutoa pole.
 
Back
Top Bottom