Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Mimi binafsi imenitokea muujiza wakati naangalia tv yake tena nilitumia maji ya kununua dukani ,cha msingi imani yako itakuponya
Kweli Mr,unajua hata mahali Fulani Kristu mwenyewe alikataa kufanyia miujuza kwa Mafarisayo,wengine kwa Imani wanaomba uponyaji na utatuzi.ila wengine wanahitaji mazingaumbwe ambayo kwa Yesu hayapo.
 
Na degree mbili kutoka reputable institution Dunia...
Hii debate haiitaji hasira....mtu kama Mimi hapo kale unaanzaje ku nipeleka Kwa walokole.......
Nina shuuhuda nyingi sana za
Hapo kawe...
MUNGU ni mwema wakati wote...
Amina
Tupe bas walau 2 tu
 
Hata mimi nilikuwa siamini lakini naamini kwa sababu tatizo lililokuwa linanisumbua miaka mingi limeisha

Wale waganga wanakutupia halafu we we ndio unawafuata wayatoe. Shetani haponyi bali anaharibu na kutengeneza. Yesu Kristo ndio mponyaji mwamini yeye pekee.
 
Kweli Mr,unajua hata mahali Fulani Kristu mwenyewe alikataa kufanyia miujuza kwa Mafarisayo,wengine kwa Imani wanaomba uponyaji na utatuzi.ila wengine wanahitaji mazingaumbwe ambayo kwa Yesu hayapo.

Kweli kabisa, Yesu Kristo anatenda miujiza ila wengine ndio mazingaombwe yaliyobistiwa na maji na mafuta.
 
Yaani nguvu za giza unafananishia na nguvu ya Mungu?
Yuko wapi Mch. Kakobe?
 
Kumbe ulinunua mafuta kwenye vituo vyake. Jamaa kajitanua kibiashara.
Mikoa mingi kuna vituo,hata kama ungekuwa wewe mtu anafunga safari kutoka Tanga kufuata mafuta tu? Hungefikiria kurahisisha huduma?
Najua kwa Mwamposa huendi ila kwa waganga wenu wa kienyeji unaenda.Tatizo sijui nini kwako au wivu?
Suala la biashara linakuja automatically kwa sababu sio hapa Tanzania tu dunia kwenye dini kuna hela ujue hivyo.Hata wachungaji na watumishi wengi wa dini za kikristo wana hela na milionea wakubwa
Shida sio wao kuwa mailionea kama tatizo lililokupeleka limeisha
Watu wanatoa mamilioni kama sadaka ya shukrani baada ya matatizo yao kuishi. Vitu vya kufeki havikai muda,jaribu kuangalia Mwamposa toka aanze kutoa huduma miaka mingap imepita?
 
Asee acha kumfananisha YESU KRISTO na mwamposa ni kosa kubwa sana. YESU KRISTO alifanya makubwa sana mengine hayajaandikwa maana yangeandikwa yote hakika Dunia isingetosha sehemu ya kuweka vitabu vya kumuhusu. Usikufuru. [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Huu ushuhuda niliusikiliza jana kwenye Tv yake ya Arise 😁
 
Wale waganga wanakutupia halafu we we ndio unawafuata wayatoe. Shetani haponyi bali anaharibu na kutengeneza. Yesu Kristo ndio mponyaji mwamini yeye pekee.
Nakubaliana na wewe kwenye uponyaji na inawezekana pia katika makusanyiko ukapata mapepo pia.Hapa nina ushuhuda pia wa mama yangu mzazi alipata ukichaa akiwa kwenye makusanyiko huko Dar
Lakini baada ya miaka mitano amekuja kupona kwa imani pia kupitia watumishi wa Mungu lakini si Mwamposa
Tunazungumza kuhusu nguvu ya Mungu kupitia watumishi wake akiwemo Mwamposa.Mwamposa mwenyewe hana uwezo wowote ndio maana anasema " kwa jina la Yesu anayeweza" ndiye anayeleta suluhisho la shida za binadamu
 
Lakini Mwamposa siyo Nabii, ni Mtume.

Mtume unajua maana yake?. Mtume hutakiwi kuwa na Kanisa wewe ni kuzunguka dunia nzima Kama Paulo na kufungua kazi. Sasa Mwamposa wako yeye ndio kwanza amejenga hoteli ya kitalii na mashamba ya avocado. Kila siku yupo Kawe na ibada zake za kubeba sadaka. Yule sio mtume.
 
Hakuna hata mtu mmoja ameponywa chochote. Mwamposa ni muongo mlaghai kama wote wengine. Ameshaua watu 20 moshi kugombea kukanyaga uongo wake wa mafuta. Wenye misimamo hatuamini miujiza ndio tunajua. Serikali ichukue hatua kukomesha huu ulaghai na utapeli kwenye imani za kiroho. Wasisubiri hadi tuwe na mackezie wa tanzania.
 
Siamini kama watu wote wale wanapangwa.
Hivi kwani haiwezekani watu kupona Magonjwa?
Kama tunamuamini Mungu,basi tuamini pia kuwa anaponya.

Hivi kwa Mwamposa anaponya Mungu kweli?. Jiulize hilo swali. Maana ukishafanya uponyaji wa maji, mafuta na keki basi Mungu hayupo hapo, maana Mungu anajitosheleza haitaji msaada wa maji kuponya.
 

Asante, nimekuelewa mtumishi.
 
Upumbavu wa Mackenzie wa Kenya au Kibwetere wa Uganda ulianza hivihi. Labda kama wewe ni mpagani nitakueelewa lakini kwa Mkristu kuanza kumfananisha Yesu na Mwaposa hii ni KUFURU ya hali ya juu.

Yesu hakufanya miujiza kama sehemu ya kushawishi watu wamfuate au kama sehemu ya kazi yake bali aliwaponya wale aliokutana nao kwa huruma yake tu na imani yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…