Wakristo wanafundishwa toba na msamaha.. Kusamehe saba mara sabini.. Kusamehe kabla jua halijakuchwa... Lakini zaidi ya yote kusamehe na kusahau!
Tunakoseana mengi..! Tunasameheana mengi..! Tunasahau mengi tena na tena! Lakini
Kamwe hatusamehe ya makusudi
Kamwe hatusamehe ya kudhamiria
Kamwe hatusamehe ya kupanga
Kamwe hatusamehe ya kudharauliwa, kubezwa na kuchekwa!
Vita havijawahi kuamua ugomvi .. Bali meza ya mazungumzo... Lakini inategemea unazungumza na nani.. Unazungumza nini... Ili upate nini..!
Mtu aliyekudharau kwa kila hali na akakufanyia kila aina ya ubaya.. Akakutesa.. Akakuumiza.. Akakupa majeraha ya kimwili na kiroho.. Mtu ambaye ameinajisi ardhi kwa damu zisizo na hatia.. Mtu ambaye mikono yake imejaa damu unaweza kuketi naye meza moja kwa mazungumzo?
Wakati akikuomba mkae chini myajenge nyumba yake kaficha jambia
Ndugu na jamaa zako kawamaliza na kuwatupa kusikojulikana
Kawaweka wengine kwenye nyumba za siri za mateso wanaishi kama wako jehenum au akhera
Kuna wengine kawabambikia kesi za kutisha
Kakuibia haki zako za kuishi kuamua kutenda kufikiri mpaka hisia...🚯
Tuanze na uwajibikaji kabla ya maridhiano.. Waliohusika wore kuanzia juu kabisa mpaka chini kabisa wawajibishwe kila mmoja kwa uzito wake na nafasi yake.. Na hili lifanyike kwa uwazi na weledi mkubwa..
Likishakamilika hili tuitaneni sasa kwenye meza ya mazungumzo.. Na si vinginevyo...!!!!🚯🚯🚯🚯