Inahitaji ujasiri kumiliki PASSO

Inahitaji ujasiri kumiliki PASSO

Ingekuwa amri yangu ningepiga ban gari za kipuuzi zisitumike maeneo ya mjini kabisa labda mikoani huko.Exception ni kama zikiwa kwenye kampuni ya taxi na zisizidi miaka mitatu from manufactured date.

Kwa wote wenye plates za njano nahitaji kuona SUV za maana tu jijini Dar, na executive sedans, series 7 bmw, s class, royal crown, jaguar xf, ls 500 and the like! Zote zitembeazo zisizidi 5 years from manufactured date.

Sio kujaza barabara na mataka taka foleni tu za kijinga. Wasioweza wapande mwendokasi ziwekwe kila route,treni ama wanunue pikipiki!

Asanteeeeee
 
Kamanda xiro hizi gari zizuiwe kufika mjini-city centre kama zilivyo bodaboda maana zinaongeza uhalifu. Halafu ziwe mwisho saa 5 usiku. Nawasilisha.
 
Kamanda xiro hizi gari zizuiwe kufika mjini-city centre kama zilivyo bodaboda maana zinaongeza uhalifu. Halafu ziwe mwisho saa 5 usiku. Nawasilisha.
Eeh hakuna sababu ya kujaza upuuzi mjini, nashindwa elewa kwa nini mamlaka husika hazija establish standards. Sahivi ni kila mtu anajinunulia tu gari kiholela. Emission standards hazizingatiwi ila ipo day tu kuna watu wataamka na kilio cha ban ya ghafla. Si tupo!!!
 
acheni kudisi jamani wengine mnatudanganya mnamiliki sijui magari gani acheni uongo na sifa mbaya za kudisi japan wanatengeneza magari viwanda kibao kina mitsubish,daihatsu,toyota lakini watu wake wanaongoza tumia magari madogo kwa sana hizi suzuki jimny ,kei,,toyota vitz nk sasa nyie mnajidai hampendi na tena comment za huku zinazoongooza ni za wasio hata na baskeli kama hupendi passo endelea kupenda unachopenda mi mwenyewe sipendi passo kwa vigari vidogo napenda suzuki jimny adventure kwa magari makubwa SUV nazikubali cruiser v8 iwe ya diesel prado zile diesel 1GD FTV lakin hata nikiwa nazo bado ka suzuki jimny kako pale pale kuna vi ruti vidogo huwezi kwenda na v8 mafuta yanaisha bure kwa ajil ya kusukuma tani 2 na kitu bado uzito wa abiria ....vuta picha unakaa kwenye jamu masaa mawili asubuh mawili jioni si kufaidisha wenye sheli badala yake unatumia yenye unafuu hela unafanyia ishu zingine .....

mi nadhamini kula sana bora nipande jimny yangu cc 658 afu hela ambazo ningepoteza kwenye mafuta ya v8 ninunue mguu wa mbuzi kwa morombo niwe naula nikiwa kwenye jimny yangu
 
Ingekuwa amri yangu ningepiga ban gari za kipuuzi zisitumike maeneo ya mjini kabisa labda mikoani huko.Exception ni kama zikiwa kwenye kampuni ya taxi na zisizidi miaka mitatu from manufactured date.

Kwa wote wenye plates za njano nahitaji kuona SUV za maana tu jijini Dar, na executive sedans, series 7 bmw, s class, royal crown, jaguar xf, ls 500 and the like! Zote zitembeazo zisizidi 5 years from manufactured date.

Sio kujaza barabara na mataka taka foleni tu za kijinga. Wasioweza wapande mwendokasi ziwekwe kila route,treni ama wanunue pikipiki!
Yaani sie tunaopokea mshahara wa laki 5 pia mnataka tumiliki hayo marengi rover!?? Aisee Mungu anawaona [emoji30] [emoji30] [emoji30]
 
Mtuambie vizuri nyie mnaomiliki ma- BMW, V8, na the likes, mlinunua kipindi cha madili au sasa hivi! Mi kipato changu kidogo ngoja nijikusanye nijinunulie Mazda Demio, maana ndo uwezo wangu nitafanyaje.
 
Wengi humu wanaongelea ushabiki, badala ya kujibu au kuongea kitaalamu. Wengi wenu humu mnaoponda passo na mashaka hata toyo hamiliki na hamuelewi chochote kuhusu magari mnaropoka vitu vya kipuuzi bila kuwa na facts ndio tatizo kubwa la watanzania. Wengi wenu ni waendesha magari tu na si madereva( kizazi cha automatic car). Mleta mada hio passo kama ni piston 3 basi lazima itakua kimeo tu na pia kuchemsha kwa gari kunasababishwa na vitu vingi huenda hio rejeta yako ni chafu, peleka ikafanyiwe usafi kwenye njia zake. Kwa wale wanaohitaji kununua passo nawashauri wanunue zile zenye cc1290 ni gari nzuri sana popote unaenda na highway imetulia. Nimeshasafirisha passo nyingi tu kwenda nje ya nchi sijawah kuona zinachemsha . Ila tatizo lililopo kwenye passo ni reckhand( mkono wa stering) huo ndio ugonjwa wa passo tu na wala si ishu kubwa kivile unaweza kubadili. Na siku hizi sio dili tena kuendesha mi v8 , range na zingine dunia ya sasa watu wanaangalia economy tu hususani kwa nchi zetu zinazoendelea.
 
Tusikatishane tamaa, humu kuna vijana tunaanza maisha kuna ambao wapo kati hivyo toeni majibu ya kitaalamu tujue kwanini si vyema au ni vyema kumiliki Passo.
Mkitoa majibu ya kijiweni tutakua hatufiki.
 
Back
Top Bottom