Inahitaji ujasiri kumiliki PASSO

Inahitaji ujasiri kumiliki PASSO

Huwezi kuwa na akili timamu ukaja sehemu nikakuuliza umekujaje ukasema umekuja na gari halafu ukanionesha passo...ni bora uje na daladala tu nijue hujanunua gari unajipanga. passo nayo ni gari? hiki ni kidude kinatumika kwa wale wacheza golf kuwazungusha wenye viwanja vya golf huku tanzania ndo tunasafiria. sasa passo unaenda nayo mbeya na ile milima kweli wewe una akili? unataka upate ajali njiani umsingizie shetani..kigari kinapigwa upepo kinataka kupinduka umeshwah endesha gari njia kuu ukakutana na yale malori au mabasi yameachia break yanawah mitaa flan? ule upepo wake tu unaweza ukakuta kigari chako kinaBinduka. viacheni vipasso hapa mjini tu akina mama waendee sokoni na wadada wa kazi pia kuwapelekea watoto shule. ila usije mwanaume mzima na akili zako unanambia una gari gari lenyewe passo....jinga kabisa.

Taratibu Mkuu. Umewadisi sana mpaka wanajisikia vibaya wamiliki wa Passo.
 
Hiyo ni passo yako tu, pole me nina passo tangu 2014 mpaka leo na napiga root ndefu zote Tanzania bara. Hakuna cha kutoa thermostat wala nn na hii yangu ni 4p

Mkuu na wewe mwanaume unaendeshaje Passo? Hayo ni magari ya wanawake mkuu.
 
Bashite piga marufuku PASSO kama ulivyofanya kwa SHISHA
 
Hongera mkuu tena hongera sana ila kumbuka Mungu anakuona ujue na Mungu hanaga mdhaa. Kwa hiyo ni heri ununue baisikeli au usiwe na chombo chochote cha usafiri kuliko passo sio? Nimekuelewa mkuu

Usimaindi mkuu nilikuwa nakuchagiza tu mkuu. Hiyo pesa ya Passo changa kidogo utapata kitu cha hadhi ya juu kidogo.
 
Usimaindi mkuu nilikuwa nakuchagiza tu mkuu. Hiyo pesa ya Passo changa kidogo utapata kitu cha hadhi ya juu kidogo.
Shida yetu watanzania tunajali hadhi sana kuliko function ya chombo chenyewe... wenzetu wanao tengeneza hivi vitu hawako hivyo... kwa sasa wat i care nna fika niendako sio nionekanavyo... mzee badilika
 
b51917880d8002d381b72c0151482e29.jpg
passo wanabebea matofali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka kufikia hatua ya kumiliki gari aina ya PASSO inapaswa ujitoe ufahamu mbele ya kadamnasi. Gari gani isiyoweza kutembea 200 kms bila kuchemsha?

Nasubiria tamko/katazo la hizi gari toka ngazi za juu.
Mkuu, tumesafiri na Passo mpaka Moro Km 200 saafi kabisa. Tumetumia mafuta ya buku 22 tu! This is the car to have I tell you...
 
Mkuu, tumesafiri na Passo mpaka Moro Km 200 saafi kabisa. Tumetumia mafuta ya buku 22 tu! This is the car to have I tell you...
Nakuhakikishia MTU anayeponda gari flani hajawahi kumiliki hata baiskeli! Sina passo lkn naamini ni gari poa tu! Ilimradi siendeshei milimani najua itadumu tu bila wasi

Sent from Moto G
 
Nakuhakikishia MTU anayeponda gari flani hajawahi kumiliki hata baiskeli! Sina passo lkn naamini ni gari poa tu! Ilimradi siendeshei milimani najua itadumu tu bila wasi

Sent from Moto G

Most likely
 
Lazima kabla ya kujadili aina ya gari ni lazima tujue kuwa kila mtu hununua gari kulingana na matumizi na kipato chake, passo ni gari kama gati zingine, iwe ya cylinder 3 au 4, kikubwa ni matunzo na kufanya service kwa wakati na kutumia mafuta na spea zenye ubora

Masasaa Original
 
Back
Top Bottom