Inahitajika mtaji kiasi gani ili kuweza kufanya shughuli za uwakala wa mabenki?

Chief Kumbyambya

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2022
Posts
719
Reaction score
2,408
Habari wadau,

Kwa wale wenye uzoefu na biashara hii ya uwakala wa kibenki, yaani unakuwa na kibanda chako lakini unafanya shughuli za uwakala wa mabenki mbalimbali, kama vile NMB na CRDB inahitaji mtaji wa Tsh ngapi Ili kuifanya biashara hii bila kutetereka?

Na pia ni vitu gani muhimu vya kuzingatia ili kuifanya biashara hii kwa ufanisi zaidi?

Natanguliza shukrani zangu za dhati!
 
Mtaalam wa haya mambo, Binti mdogo kabisa mrembo na tajiri amu atakuja kutoa muongozo.

Lakini kwa huu mwendo wa ongezeko la tozo hii biashara ya uwakala wa mabenki inalipa kweli? Najua itategemeana na eneo unalotaka kufanyia hii biashara nikimaanisha mzunguko na pia ukubwa wa mtaji wako.
 
Mtaalam wa haya mambo, Binti mdogo kabisa mrembo na tajiri amu atakuja kutoa muongozo.

Lakini Kwa huu mwendo wa ongezeko la tozo hii biashara ya uwakala wa mabenki inalipa kweli? Najua itategemeana na eneo unalotaka kufanyia hii biashara nikimaanisha mzunguko na pia ukubwa wa mtaji wako.
Itakuwa safi sana akija kutoa muongozo....

Kwenye tozo hapo ndiyo shida lakini ni kukomaa nazo tu..
 
Hizi biashara za kuigana zimejaa kila kona
Bora utafute aina nyingine na kwenda na wakati
Tuwe wabunifu
Unisamehe bure
Hakuna biashara ambayo wewe utakuwa ni wa kwanza kuifanya. Chochote unachokifanya jua kwamba kuna mtu alishawahi kufanya na pengine wewe ndiyo utakifanya kwa ustadi zaidi ya waliotangulia hivyo usiogope.

Cha muhimu ni kuboresha ya kwako ili kutumia mapungufu ya wengine.
 
Hakuna biashara ambayo wewe utakuwa ni wa kwanza kuifanya.

Chichote unachofanya kuna mtu alishawahi kufanya na pengune wewe ndiyo utakifanya kwa ustadi zaidi.

Cha muhimu ni kuboresha ya kwako ili kutumia mapungufu ya wengine.

Kuna biashara nyingi sana duniani ambazo hamzijui na wewe ndio wa kuianzisha au kuiga

Usiseme Hakuna zipo nyingi sana na nitakupa mifano

Hata sehemu zilizokuwa hazina maendeleo walianza kwa vitu ambavyo vilikuwa havipo kwa kuiga mijini na kupeleka wilayani au hata miji kwa miji

Tatizo letu biashara moja kila mmoja anawaza hiyo hiyo ndio maana unakuta mmepangana miaka kibao na maisha ni yaleyale hakuna wa kutoboa

Biashara zipo Mkuu na kuiga kupo sana ila unafungua biashara ambayo itakupeleka mbele kwa faida nzuri na kuikuza pia

Fursa nyingi na kuiga iga ila uwe umeiona nchi nyingine na kuileta home
 
Labda ufungue kiwanda ndio kidoogo utakuwa hujaiga ila biashara nyingine sema cha kuzingatia labda location

Mkuu sio lazima kiwanda

Kuna fursa nyingi tu kama una hela

Vijana wengi hawajui savings na wanafanya kazi sana tu ila hawaweki ili waje kufanya kitu cha faida zaidi au kikubwa zaidi

Kwa mfano hawaweki malengo ya miaka 10 ila wanakaa na kuwa wakala kwa miaka 10 kwenye kibanda na hajiongezi na kusema niweke malengo baada ya miaka 10 nifanye kitu kingine kabisa na kikubwa na faida kubwa
 
Biashara ya Uwakala wa benki, mtaji wake inategemeana na mzunguko wako. Wateja wako ndiyo wataamua ni kiasi gani cha mtaji kiasi gani uwekeze.

Lakini ukitaka kufanya kwa ufanisi, walau uwe na 20m.

Vitu vya kuzingatia ni namna ya kuulinda mtaji wako. Iwe ni kuepuka wizi, kutapeliwa na kupata hasara zinazoepukika, mfano pesa bandia nk

Swala la pili, uaminifu. Hili jambo lilipaswa kuwa la kwanza lakini mtaji wako ni muhimu zaidi. Kuwa mwaminifu kwa mteja na Mungu pia. Usimuibie mteja au kumtoza gharama zisizokuwepo. Mfano, kumpa mteja hela ambayo haijatimia au kumpa hela ambayo ni bandia. Pia, kumtoza mteja gharama za ziada. Malipo ya serikali (GePG) hayana faida, lakini si vema kumtoza mteja. Ni bora kutokufanya kuliko kumpandikiza mteja gharama zisizotakiwa.

Tatu, jenga mahusiano bora na mawakala wenzako. Wajue mawakala wako Wakuu. Ili uwe unasaidika kwa haraka. Mteja anakuja kuweka mf 10m, huna kwa wakati huo. Usimuambie sina. Mpigie wakala wako Mkuu akuwekee, kisha umpelekee Cash. Unahitaji kuzoeleka kwanza kabla ya kupata favor hiyo.

Nne, jua aina ya miamala na faida zake. Kuna miamala yenye malipo mazuri haswa ya kutoa na kuweka, manunuzi ya umeme, vocha, nk. Kuna yenye malipo kiduchu, haswa GePG. Achana na malipo kama unaona itanyonya float yako.

Tano, fuata taratibu za kibenki zinavyoelekeza. Wateja wa kutoa wakuonyeshe kitambulisho au wajaze form kabisa. Hii itakusaidia kuepukana na risks za hapa na pale. Utazijua ukiingia humo.

Nitarejea kama kutakuwa na maswali
 
Biashara ya Uwakala wa benki, mtaji wake inategemeana na mzunguko wako. Wateja wako ndiyo wataamua ni kiasi gani cha mtaji kiasi gani uwekeze.

Lakini ukitaka kufanya kwa ufanisi, walau uwe na 20m.

Vitu vya kuzingatia ni namna ya kuulinda mtaji wako. Iwe ni kuepuka wizi, kutapeliwa na kupata hasara zinazoepukika, mfano pesa bandia nk

Swala la pili, uaminifu. Hili jambo lilipaswa kuwa la kwanza lakini mtaji wako ni muhimu zaidi. Kuwa mwaminifu kwa mteja na Mungu pia. Usimuibie mteja au kumtoza gharama zisizokuwepo. Mfano, kumpa mteja hela ambayo haijatimia au kumpa hela ambayo ni bandia. Pia, kumtoza mteja gharama za ziada. Malipo ya serikali (GePG) hayana faida, lakini si vema kumtoza mteja. Ni bora kutokufanya kuliko kumpandikiza mteja gharama zisizotakiwa.

Tatu, jenga mahusiano bora na mawakala wenzako. Wajue mawakala wako Wakuu. Ili uwe unasaidika kwa haraka. Mteja anakuja kuweka mf 10m,huna kwa wakati huo. Usimuambie sina. Mpigie wakala wako Mkuu akuwekee, kisha umpelekee Cash. Unahitaji kuzoeleka kwanza kabla ya kupata favor hiyo.

Nne, jua aina ya miamala na faida zake. Kuna miamala yenye malipo mazuri haswa ya kutoa na kuweka, manunuzi ya umeme, vocha, nk. Kuna yenye malipo kiduchu,haswa GePG. Achana na malipo kama unaona itanyonya float yako.

Tano, fuata taratibu za kibenki zinavyoelekeza. Wateja wa kutoa wakuonyeshe kitambulisho au wajaze form kabisa. Hii itakusaidia kuepikana na risks za hapa na pale. Utazijua ukiingia humo.

Nitarejea kama kutakuwa na maswali
Elimu nzuri sana hii
 
Labda ufungue kiwanda ndio kidoogo utakuwa hujaiga ila biashara nyingine sema cha kuzingatia labda location
Kuna biashara kwa mfano zimeanzishwa let say ziko Dar es salaam lakini Iringa/Mbeya haziko so inabidi wewe uwe wa kwanza kuanzisha katika hiyo location ya Mbeya/Iringa huu ndio ubunifu uanaotakiwa na sio kuiga biashara ambayo kwenye kila vichochoro zimejazana.
 
Kuna biashara nyingi sana duniani ambazo hamzijui na wewe ndio wa kuianzisha au kuiga

Usiseme Hakuna zipo nyingi sana na nitakupa mifano

Hata sehemu zilizokuwa hazina maendeleo walianza kwa vitu ambavyo vilikuwa havipo kwa kuiga mijini na kupeleka wilayani au hata miji kwa miji

Tatizo letu biashara moja kila mmoja anawaza hiyo hiyo ndio maana unakuta mmepangana miaka kibao na maisha ni yaleyale hakuna wa kutoboa

Biashara zipo Mkuu na kuiga kupo sana ila unafungua biashara ambayo itakupeleka mbele kwa faida nzuri na kuikuza pia

Fursa nyingi na kuiga iga ila uwe umeiona nchi nyingine na kuileta home
Umesema utatoa mfano wa hiyo biashara ya bila kuigana. Nausubiri mfano mtaalam.
 
Biashara ya Uwakala wa benki, mtaji wake inategemeana na mzunguko wako. Wateja wako ndiyo wataamua ni kiasi gani cha mtaji kiasi gani uwekeze.

Lakini ukitaka kufanya kwa ufanisi, walau uwe na 20m.

Vitu vya kuzingatia ni namna ya kuulinda mtaji wako. Iwe ni kuepuka wizi, kutapeliwa na kupata hasara zinazoepukika, mfano pesa bandia nk

Swala la pili, uaminifu. Hili jambo lilipaswa kuwa la kwanza lakini mtaji wako ni muhimu zaidi. Kuwa mwaminifu kwa mteja na Mungu pia. Usimuibie mteja au kumtoza gharama zisizokuwepo. Mfano, kumpa mteja hela ambayo haijatimia au kumpa hela ambayo ni bandia. Pia, kumtoza mteja gharama za ziada. Malipo ya serikali (GePG) hayana faida, lakini si vema kumtoza mteja. Ni bora kutokufanya kuliko kumpandikiza mteja gharama zisizotakiwa.

Tatu, jenga mahusiano bora na mawakala wenzako. Wajue mawakala wako Wakuu. Ili uwe unasaidika kwa haraka. Mteja anakuja kuweka mf 10m,huna kwa wakati huo. Usimuambie sina. Mpigie wakala wako Mkuu akuwekee, kisha umpelekee Cash. Unahitaji kuzoeleka kwanza kabla ya kupata favor hiyo.

Nne, jua aina ya miamala na faida zake. Kuna miamala yenye malipo mazuri haswa ya kutoa na kuweka, manunuzi ya umeme, vocha, nk. Kuna yenye malipo kiduchu,haswa GePG. Achana na malipo kama unaona itanyonya float yako.

Tano, fuata taratibu za kibenki zinavyoelekeza. Wateja wa kutoa wakuonyeshe kitambulisho au wajaze form kabisa. Hii itakusaidia kuepikana na risks za hapa na pale. Utazijua ukiingia humo.

Nitarejea kama kutakuwa na maswali
Shukrani sana mtaalam kwa haya madini. Vipi nikianza na mtaji wa Tsh. 2,000,000/= naweza kuifanya biashara hii kikamilifu kwa mategemeo ya mtaji kuongezeka mbeleni!!?
 
Umesema utatoa mfano wa hiyo biashara ya bila kuigana. Nausubiri mfano mtaalam.

Nafikiri franchise hakuna sana huko
Tunaona watu wengi wanakokota pikipiki kwa kuishiwa mafuta (petrol) au hata magari kuishiwa diesel/petrol

Sasa unakuwa na tank kwenye gari kama pickup na unakuwa na simu yako au app kwa wahitaji wako
Najua haipo sana huko au Hakuna kabisa ila inalipa

Kuna business idea nyingi sana online Mkuu unaweza kuziangalia wewe na kuchagua ipi inakufaa kwani zipo ambazo hazihitaji hata mtaji bali wewe tu

Naweza kukupa mifano ila unaweza ukawa huna mpango nao ila ukijisomea utaamua mwenyewe

Wenzetu ni opportunist ikitokea kitu tu wanaichangamkia

Kwa mfano huku zimeingia sana na kutengenezwa gari za Umeme ila charge zake sio nyingi hivyo
Tatizo linakuja kwa mtu anaishi gorofani na hawezi ku charge
Hapo wakajiongeza
Kampuni zimeanza wanakuja kucharge kwako na unawalipa
Hii ni moja ya mfano wa biashara ambayo ilikuwa haipo

Leo magari mengi mapya lazima uweke Adblue na hii itakuja tu huko miaka sio mingi
Je wataalamu wetu wale wa PHd zao watatengeneza Adblue ili tuuze nchi zingine au watasema iwe imported toka Kenya? Wakati ni rahisi sana kuitengeneza

Mkuu tusaidiane kwa biashara na humu wapo wengi wanazijua pia
 
Biashara hizi ukiwa unaomba uwakala wanahitaji tu uwe na kianzio cha 2M ndipo wakupe machine (Pos)

Kwa ushauri ili uweze kumudu hizi biashara lazima uzingatie hivi.

1. Mtaji
  • Walau ukiwa na 10M itakusaidia kwa mzunguuko wa siku nzima haitokupeleka bank mara kwa mara kutoa float au kuchukua float.
  • Hata mteja akihitaji kutoa ama kuweka 2M asiwe anakosa.

2. Eneo (Watu)
- Hakikisha eneo unalofanyia biashara hii kuna mzunguuko mkubwa wa watu ikiwa na mana kwamba watu ni wengi sana eneo hilo.

3. Huduma
- Siku zote mteja anahitaji kujaliwa hapendi anataka huduma wewe una chat na simu badala yake akihitaji huduma unamsikilza na kumhudumia chap chap.

#Ukizingatia haya
Amini nakuthibitishia hata mkipanga mawakala zaidi ya watano biashara utaifanya tu.
 
Shukrani sana mtaalam kwa haya madini. Vipi nikianza na mtaji wa Tsh. 2,000,000/= naweza kuifanya biashara hii kikamilifu kwa mategemeo ya mtaji kuongezeka mbeleni!!?
Mkuu hii hela yako ni ndogo, tqfuta 10m, ili uweze kupata mzunguko mzuri. La sivyo utakua unarudisha wateja na watakuzoea mwisho wa siku watajua pale nikienda siwezi pata huduma ya fedha nyingi, unaishia kuua biashara.
 
Nafikiri franchise hakuna sana huko
Tunaona watu wengi wanakokota pikipiki kwa kuishiwa mafuta (petrol) au hata magari kuishiwa diesel/petrol

Sasa unakuwa na tank kwenye gari kama pickup na unakuwa na simu yako au app kwa wahitaji wako
Najua haipo sana huko au Hakuna kabisa ila inalipa

Kuna business idea nyingi sana online Mkuu unaweza kuziangalia wewe na kuchagua ipi inakufaa kwani zipo ambazo hazihitaji hata mtaji bali wewe tu

Naweza kukupa mifano ila unaweza ukawa huna mpango nao ila ukijisomea utaamua mwenyewe

Wenzetu ni opportunist ikitokea kitu tu wanaichangamkia

Kwa mfano huku zimeingia sana na kutengenezwa gari za Umeme ila charge zake sio nyingi hivyo
Tatizo linakuja kwa mtu anaishi gorofani na hawezi ku charge
Hapo wakajiongeza
Kampuni zimeanza wanakuja kucharge kwako na unawalipa
Hii ni moja ya mfano wa biashara ambayo ilikuwa haipo

Leo magari mengi mapya lazima uweke Adblue na hii itakuja tu huko miaka sio mingi
Je wataalamu wetu wale wa PHd zao watatengeneza Adblue ili tuuze nchi zingine au watasema iwe imported toka Kenya? Wakati ni rahisi sana kuitengeneza

Mkuu tusaidiane kwa biashara na humu wapo wengi wanazijua pia
Hyo ya Gari nyanda za juu kusini ishaingia kitambo sana (Mobile Petrol station) kuna jamaa ana magari yake kwa wilaya mbarali anazunguka sana na kujaza mafuta.
Alaf mtu anapoimba ushaur toa pasipo kukatisha tamaa kama mtu yupo Dar na anataka afanye yeye mwenyewe unamwambiaje akafungue iringa au mbeya?
 
Back
Top Bottom