Inakosekana kanuni au sheria ya kuiadhibu klabu inapotangaza haitacheza mchezo ulio katika ratiba

Inakosekana kanuni au sheria ya kuiadhibu klabu inapotangaza haitacheza mchezo ulio katika ratiba

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Kimsingi, hauwezi kumuadhibu mtu au taasisi kwa sheria au kanuni ambayo haipo.

Kwenye sakata la derby ya Yanga vs Simba ambalo tumekuwa nalo kwa miezi kadhaa sasa, imetuonyesha mapungufu ya kanuni mbalimbali za uendeshaji wa ligi na adhabu zake.

Tukiacha yote hayo, moja ya mapungufu makubwa ni kukosekana kwa kanuni ambayo inaweza kuiadhibu klabu au kiongozi wa timu inapotamka au kuchapisha kauli ya kusema hawatacheza mchezo fulani uliopangwa katika ratiba.

Kukosekana kwa kanuni hiyo na adhabu yake ndiyo kulipelekea Simba kusema hawatacheza mchezo wa 08/03 na baadae kujificha katika kichaka cha taarifa ya Bodi ya Ligi kuahirisha mechi iliyotoka mchana wa siku ya mchezo.

Simba hawawezi kuadhibiwa kwa kutopeleka timu uwanjani kwa sababu Bodi ya Ligi ilikuja kuahirisha mchezo na hakuna anayejua au aliye na uhakika iwapo Simba kweli ingesimama katika kauli yake na isingepeleka timu uwanjani siku ile iwapo Bodi yenyewe isingeahirisha mchezo. Lakini kitendo cha kutoa tu taarifa ya kutocheza mchezo ilitakiwa iwe na adhabu yake.

Yanga nayo imekuja kupita mule mule katika mapungufu haya. Kila wanapotoa matamko wanasema "HATUCHEZI". Hii nayo inazua taharuki na kama ilivyokuwa kwa Simba, hakuna aliye na uhakika iwapo kweli Yanga haitapeleka timu uwanjani siku iliyopangwa mchezo kufanyika.

Kutokuwepo kwa sheria au kanuni hii kutaibua mbinu mpya ya kishamba ya timu mbalimbali kutafuta kijisababu halafu kujitamkia kuwa haitacheza mchezo ili kuathiri mapato ya timu mwenyeji au kumfanya asijiandae kimbinu na kisaikolojia halafu kumshtukiza kwa kupeleka timu uwanjani.

TFF na Bodi ya Ligi wana kazi kubwa ya kufanya mwishoni mwa msimu kufumua mfumo mzima wa uendeshaji wa ligi.

Naona kama Tanzania imepata UFUNUO mpya maana kila sehemu sasa kelele za mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji, kuanzia kwenye Katiba ya nchi, uchaguzi hadi kwenye mpira, zimekuwa kubwa sana na watu hawataki kucheka na wowote. Kule watu wanataka tume huru ya uchaguzi, huku watu wanataka bodi huru ya ligi.
 
Kucheza Na Ratiba ni vitu viwili Tofauti.
Hao wameigomea ratiba lakini sio Mchezo husika.

Huwa wanasema huwezi kuvuka mto kabla hujaufikia.
 
Back
Top Bottom