Inakuaje akaunti ya M-Pesa ya CHADEMA inasema pesa zimejaa wakati kwenye makubaliano Vodacom ilisema akaunti haina ukomo?

Inakuaje akaunti ya M-Pesa ya CHADEMA inasema pesa zimejaa wakati kwenye makubaliano Vodacom ilisema akaunti haina ukomo?

Kisasi kama hicho ni hatari kwa ustawi wa taifa.
Lazma kisasi kitakuwa kikali zaidi ya DOGE. Nchi itapona kwa muda kabla ya mambo kuparanganyika tena baada ya rushwa nzito nzito kutembezwa kwa mawakala wa serikali.
 
Kumbe chawa wa mom wako mpaka voda😂😂😂😭
Chawa wako kila kona na wazee wa kaunda suti aka Maelekezo wako mpaka huko Vodacom na wanajua wanachotakiwa kukifanya kupitia maagizo toka juu.
 
Propaganda za kipuuzi kabisa hizi. Kama akaunti imejaa pesa tuonesheni ni shilingi ngapi zimo humo! Lissu HANA ubavu wa kuchangisha zaidi ya milioni kumi. Ushahidi ni michango ya gari lake.
Kwani hiyo message imetoka CDM, si imetoka VODA?
 
Watu wengi wameeleza kushindwa kuichangia CHADEMA kupitia mtandao wa Mpesa/Vodacom.

Baadhi ya waliojaribu kuwasiliana na Vodacom huduma kwawateja, wameambiwa kuwa eti akaunti hiyo ya CHADEMA imejaa pesa, na hivyo haiwezi kupokea hela zaidi. Wakati kwenye makubaliano kati ya CHADEMA na Vodacom, akaunti hiyo ya CHADEMA, haina ukomo wa kupokea pesa.

Hivyo kushindwa kupokelewa pesa kutoka kwa wadau wa CHADEMA inaonekana ni mpango uliosukwa kati ya Vodacom na mahasimu wa CHADEMA, kwa nia ya kuihujumu CHADEMA.

Kweli CCM ni chama cha uharibifu wa kila eneo!!!

Muda si mrefu, viongozi wa CHADEMA watatoa tamko kuhusiana na uharamia huu wa kampuni ya Vodacom.

View attachment 3254909

Pia soma: Vodacom yatolea ufafanuzi Malalamiko ya Ukomo wa Kupokea pesa kupitia huduma ya Mpesa
Wafungue akaunti zaidi ya moja, ikijaa hii, unatuma kwenye akaunti nyingine
 
Hivi ni tangu lini bank huwa inasema imejaa mapesa na haitaki tena watu waendelee kuyaweka? Hiyo Vodacom ni kama bank ( ya mtandao) sasa inaposema kwamba account imejaa, malimbikizo ni shilingi ngapi ? utopolo mtupu...
Hapo umeshajiona umeandika point. Mpuuzi sana wewe.
 
Duh,mbona za kina Mwamposa na Jodevi hazijai?
 
Wahasibu wao dio bogus, kama imejaa si mnatoa au kuhamisha kwenda bank within seconds tu?? Mbona kama propaganda? Vodacom wajibu hili officially kuondoa sintofahamu! Tutaona mengi bado..
 
Propaganda za kipuuzi kabisa hizi. Kama akaunti imejaa pesa tuonesheni ni shilingi ngapi zimo humo! Lissu HANA ubavu wa kuchangisha zaidi ya milioni kumi. Ushahidi ni michango ya gari lake.
Mjinga mmoja wewe. Umeambiwa pesa ya chadema na kampuni ya vodacom .LISU ameingiaje hapa. Haya one mkubwa wewe.
 
Siwezi shangaa kwa hili!

Kama ukumbi tu walifanyiwa figisu na kule alipokwenda kiongozi wa Chadema Toka Zenji mkutano ulizuiwa kwa mtutu wa mabunduki

Hivyo hili si ajabu kabisa

Hawa mashetani wa Chama Cha Mashetani, chini ya mama, hakuna baya wanaloshindwa kulifanya. Kama walimwua Ally Kibao na wengine wengi, na wengine kuwateka na kuwapoteza/kuwaua, kuna ushenzi gani watakaoshindwa kuufanya!!!
 
Wahasibu wao dio bogus, kama imejaa si mnatoa au kuhamisha kwenda bank within seconds tu?? Mbona kama propaganda? Vodacom wajibu hili officially kuondoa sintofahamu! Tutaona mengi bado..

Wewe unaamini kuwa account imejaa!! Hayo ni maneno tu ya kutaka kuficha uovu wao. Vodacom inaonekana wameblock hela usiingie kwenye hiyo account.
 
Hapo umeshajiona umeandika point. Mpuuzi sana wewe.

Mbona wewe ndiye unaonekana mpuuzi!! Hujibu hoja, unabakia kuropoka.

A counts zote za fedha kwenye mitandao huwa kuna makubaliano kati ya mtandao na mteja.
 
Serikali ipitishe sheria ya kuzuia vyama vya siasa kuchangisha hela
Wanaochanga wanafanya hivyo kwa hiari yao.
CCM inaiba pesa za walipa kodi bila ya hiari yao.

Tuzuie wizi wa CCM, tufute na ruzuku kwa vyama vya siasa. Vyama vie deshwe kwa michango ya wanachama.
 
Mbona wewe ndiye unaonekana mpuuzi!! Hujibu hoja, unabakia kuropoka.

A counts zote za fedha kwenye mitandao huwa kuna makubaliano kati ya mtandao na mteja.
Chini ya sheria ipi ndugu? Fedha haziwekwi hovyo kwenye account bila kufuata sheria.
 
Nadla

Hujui ulichohamaki na kujibu. Hawajasema Lissu amekusanya nini, wamesema mfumo umechezewa

Nina hakika umehamaki kujibu kisichoelezwa na mtoa mada. Ama hujamuelewa au chuki zako. Hawajasema chochote kuhusu Lissu au kiwango kilichochangiwa. Wamelalamikia hujuma Account kugoma kupokea pesa kwa kisingizio cha Account kujaa pesa. Hata mimi ningejiuliza, kwani Account zingine zimewahi kukataa pesa kwa kisingizio kama hicho? Hatukosei kusema ni hujuma za kitoto japo zitawakwamisha hao Chadema.
Una uelewa wowote wa masuala ya akaunti za M Pesa za Vodacom?
 
Back
Top Bottom