Inakuaje Lawrence Mafuru azikwe Dar na sio kwao Mara?

Inakuaje Lawrence Mafuru azikwe Dar na sio kwao Mara?

Nikiangalia ratiba ya mazishi ya poti Mafuru, inaonyesha atazikiwa Dar. Kwa kumbukumbu zangu huyu ni mtu wa mkoa wa Mara huko, na kawaida ya watu wa Mara huwa hawazikiwi nje ya mkoa wao.

Sasa najiuliza huyu bwana imekuaje azikiwe huko Daslamu na wakati ana kwao?

Pia soma TANZIA - Lawrance Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango afariki dunia

Hayo ni mambo ya kifamilia. Kuzikwa nayo haijawa ni issue ya kitaifa. Kunawatu wengi wanazikwa Dar na wanatoka mikoani
 
Mada fikirishi hii, kila mmoja inamgusa kwa aina yake; wengi hatuna tamaduni ya kupaweka sawa kwenye vijiji vilipotoka vizazi vyetu.
Wengi huwa tunawekeza sana, pale panapotupatia mkate wa kila siku.
 
In Africa, we don't die, tunakuwa ancestors, sasa imagine unakuwa ancestor makaburi ya kisutu au kinondoni, koshoto na kulia umezungukwa na strange spirit is, hazioani na mizimu yenu, mwingine kafa kwa kupigwa mawe baada ya kuiba simu, mwingine alikuwa changudoa. Unamzika hapo, number kuna mtu mwingine alizikwa eneo hilo, spirit yake bado iko hapo inarandaranda.

Hata mkienda kumuombea, mnajikuta mnaombea kitu kingine.

Lastly, ni uchawi, wengi wanaogopa kupeleka familia zao vijijini kwa sababu ya uchawi. Hasa kwa wajita, wakerewe na wakwaya, na wajaluo. Wakurya uchawi si sana, wao ni kukatana mapanga tu.
Hiyo paragraph ya mwisho inasikitisha sana
 
Wabongo Bwana, kwani lazima kuzikwa kijijini walikotoka babu zako?.

Kama babu na Baba zako walishindwa kupajenga wewe ni nani uweze kupajenga, ukijaaliwa sawa na usipojaaliwa ni sawa pia.

Hivi ni lazima ukijenga Dar au kwingineko na kijijini kwenu pia ukajenge nyumba nzuri?
Tuna uhakika gani na kipato cha mtu mpaka tumlazimishe akajenge kwao.
 
Siyo lazima. Mambo yamebadilika sana. Ndoa nyingi zimekuwa za makabila tofauti. Junior (watoto) wengi hawajui kwao. Utazikwa na kaburi watalisahau
 
Back
Top Bottom