Lazima nicheke kabla ya kukupa pole🤣🤣😌😌 .
Mpangilio wa uandishi wako umejenga taswira ya clip inayocheza kuonesha tukio halisi.
Mkuu huyo ni indivisual mmoja anayeakisi tabia halisi za waTz walio wengi, huo ni utamaduni wetu kwa sasa kutokana na utawala uliopo madarakani.
Huyo mtu akifukuzwa kwene hako kaofisi, hana ujanja wowote wa kuvimba, ni sawa na rundo la kuku waliochinjwa na kunyonyolewa manyoya, hukosa utambulisho.
Thibitisha niyasemayo kwa kuangalia utendaji wa watumishi kwenye mnyororo wa vyombo vya kutolea haki ama kusimamia sheria.
Pia angalia sehemu za kutolea huduma za afya za umma na nyinginezo za kijamii nk nk, ni uozo mtupu wa jinsi hiyo.
Tukija kule juu kwenye 'top layer', ndiyo usiseme, wanaambiwa wale pole pole bila wasi wasi tena kwa urefu wa kamba zao walizosetiwa shongoni na mmiliki wao.
Sisi raia tumekosa mwakilishi wa kuweza kututetea.
Wanaoitwa wawakilishi na kile wanachokiwakilisha ni tofauti na shida pamoja na dhiki zetu.
Kiuhalisia hii Serikari inatakiwa tatally overhall kwa sanduku la kura ama kwa umwagaji wa damu ili kurudisha heshima iliyokwisha kupotea.