Na hapo kumbuka Israel inapigana kwa tahadhari ku target zaidi magaidi ili kupunguza casualities za civilians zisizokwepeka, ni tofauti na nchi hizi zingine ambazo hushambulia zaidi raia wa kawaida wa Israel, lengo lao huwa ni kuua raia wa Israel wengi kadri inavyowezekana...
Unaonekana umemeza sana stori za vijiweni pia HUNA UNACHOJUA kuhusu mzozo wa mashariki ya kati.
-Tukianzia na six days war ya 1967 ilopiganwa tarehe 5-10 kama sijakosea February.
Hakuna mataifa ya kiarabu yaliyoungana dhidi ya Israel,bali kulikua kuna kujiandaa kwa mataifa ya kiarabu hususan Egypt na Syria.
Egypt ilinunua ndege vita takriban 200 za Kisovieti na Syria ilikua ikijiimarisha kijeshi ili waje kuishambulia Israel kwa kushtukiza na kwa pamoja.Ila isivyo bahati Israel waligundua mipango na kupiga Kambi ya jeshi la anga la Egypt uliokuwepo Sinai na kuteketeza ndege zote 200 kesha na kuiteka Sinai.
Ila Syria ndio ilishambuliwa sana na ndege vita za Israel na kuporwa Gollan heights,Rais wa US wa kipindi kile ndiye aliyeiamuru ISRAEL isitishe mashambulizi ya anga ndio vita ikaisha February 10.Kilichotokea ni mashambulizi ya anga ya Israel ila sio vita kamili kati ya waarabu na Israel.Usisahau 1973 kuna vita ilopiganwa Israel ikapigwa na kuondolewa Sinai na askari wa Egypt,na katika vita ambazo Israel ilipoteza askari wengi kama mateka basi ni hiyo.
-Situation ya sasa iliyoanzia October 7 mwaka jana Israel ilipovamiwa na Hamas US Navy walituma battleship ikiwa na Navy seal wasiopungua 2000 wakiwa na ADS na silaha nyingi za kuisapoti Israel dhidi ya Hamas.
UK na Germany nao walituma msaada wa kijeshi kwa Israel,ndipo mataifa ya kiarabu walipoona mataifa makubwa yanaisaidia Israel dhidi ya kundi dogo lenye wapiganaji elfu 30 nao wakaamua kuiunga mkono Hamas kwa wanavyojua wao.
-Houthi Yemen waliamua kufunga red sea ili meli za mizigo zisiende Israel.
-Hizbollah waliamua kuipiga Israel kaskazini ili kuipunguza kasi isiishambulie sana Hamas,na kweli Israel ilipungua kasi maana Galilee raia wote wamehama na pia askari wengi kufa na kujeruhiwa.
-Iran Netanyahu alikataa kuhusika na kifo cha Rais wao alikataa kata kata,sasa utuambie wewe mkaazi wa Kimara bonyokwa ushahidi wa Israel kumuua rais wa Iran umetoa wapi ilhali Netanyahu amekataa!?
Hakuna mataifa yaloungana kumchangia Israel uwe unafuatilia taarifa sio kuropoka.
-2006 kuna vita baina ya Lebanon na Israel ilitokea na Israel alipigwa na kupokonywa Bint jubeir na sehemu ya mpaka wa bahari.Je unaijua hii vita?
Inajulikana kama operation bint jubeir.
Nimalizie tu na hivi vita vya sasa,hasara iliyopata Israel kwa kupigana na Hamas;
-Vifo vingi vya wanajeshi kiasi kupata uhaba wa wanajeshi na kulazimisha raia kuingia jeshini.
-Askari takriban 12000 kupata ulemavu wa kudumu.
-Raia takriban laki mbili kupata ukimbizi wa ndani hususan waliokua wakikaa kaskazini mwa Israel.
Cha kuongezea kama vita ya Hamas Israel ilitumia takriban silaha zake zote na kutumia wanajeshi laki tatu ili kupigana na wanamgambo elfu thelathini,je Iran yenye kila aina ya silaha ingeamua kuipiga Israel ingekuaje!?
Pia nadhani huijui Iran vizuri.
Kafuatilie vita ya IRAN-IRAQ war ilopiganwa 1980-1988 Iran ikichangiwa na Iraq na USA ila Iran ikashinda vita.
Israel bila ya USA,UK na EU sio taifa.