Inakuaje!

Inakuaje!

Hivi kwanini tunapenda kumsingizia shetani?
Kuna mtu alikuwa kila siku anamsingizia shetani mwisho mkewe akamuuliza shetani wako ni huyuhuyu aliyemuasi Mungu? akamwambia huyu shetani naona sio huyo ni mwingine kamuasi shetani original

Lizzy kama kila kitu kiko sawa including mambo ya sita kwa sita basi inakuwa ni tabia ya mtu, na wa aina hii kuacha huwa hawawezi mpaka makubwa yawapate ndio hutulia tuli.
 
Lizzy,

Huo ndio ukweli halisi wa maisha. Binadamu hana tamaa tena na kitu chake. Ni kama unavyotamani chakula cha jirani yako ukiwa hotelini. Pia waswahili wanasema kwamba samaki wako uliyekwishamvua na kumweka kwenye kikaango huwezi tena kumlisha chambo. Na kuku wako mwenyewe huwezi kumlenga manati. Siku zote watu wanatafuta ziada ingawa hawajui watakachokipata. Na huo ndio ukweli.

Kwa wale tuliojitahidi kuridhika na kile tulichonacho bado tuna mapambano makubwa ndani yetu. Niamini mdogo wangu..siyo kazi rahisi kuishi maisha ya useja katika ndoa (mke mmoja au mume mmoja). Mnaweza kunikosoa lakini...Macho hayaoni tena labda na akili pia!!

Mzee DC (1947).
 
shetani tu kawapitia, siku yao itafika wataumbuka.
Oh puhleeez!Huyo shetani wa watu hua anawapitia wangapi at once?Na anapowapitia wao wanaangalia wapi mpaka wafuate mkumbo bila kusogea pembeni wampishe huyo shetani apite??Mambo mengine tukubali tu kuchukua lawama kwasababu ni matendo yetu..hata mtu akikushawishi kitu unaweza kuchagua kutokushawishika achilia mbali kudanganywa na shetani.
 
Hivi inakuaje mwanamke anaondoka nyumbani kwake anamuaga mume wake ambae ni mzuri as in hamnyanyasi na anajitahidi siku zote kumfanyia mke yaliyo mema..alafu anaenda kukutana na kimada wake ambae nae ni mume wa mtu ambae nae mke wake anajitahidi kumfanyia yaliyo mema?Yani wote wanavunja ahadi zao kwanza kwa kutoka nje ya ndoa zao alafu wanafikia kutamani mpaka kutembea na mume/mke wa mwingine!Watu hawa ambao kuna watu wanawaangalia kama 'rolemodels' kwenye maswala ya maisha tuwachukulieje?
Ushaolewa Lizzy???
 
...mnh, watu hawa ni role models kwenye maisha ya ndoa, au maisha kwa ujumla?

Maisha kwa ujumla...ndoa included!Maana sio kila mtu anajua walivyo kweli bali wanaonyesha vile wanavyotaka kuonekana!
 
Ni kuondoka kwa hofu ya Mungu, kuporomoka kwa maadili na kukosa uvumilivu.....Mungu atusaidie....manake kama alivyosema Mbu,kwa wengi hayo ndo maisha ya kawaida....!😛layball:

Kuna haja ya kumwomba YESU arudi kabla ya muda aliopanga!
 
Kuna mtu alikuwa kila siku anamsingizia shetani mwisho mkewe akamuuliza shetani wako ni huyuhuyu aliyemuasi Mungu? akamwambia huyu shetani naona sio huyo ni mwingine kamuasi shetani original

Lizzy kama kila kitu kiko sawa including mambo ya sita kwa sita basi inakuwa ni tabia ya mtu, na wa aina hii kuacha huwa hawawezi mpaka makubwa yawapate ndio hutulia tuli.

Gaga,

Hayo mambo ya chumbani ni vitu vidogo sana kwa mtu mkware. Bado atataka kufanya sampling kuona kama quality ya nyama ni ile ile katika butcher nyingi iwezekanavyo. Labda hii kitu inatumia kanuni za statistics...kuongeza sample size kadri inavyowezekana!
 
AD kweli inasikitisha!Anayokushauri usifanye yeye anafanya zaidi...kama mtu ameamua kua mtu wa ajabu awe tayari kuonekana wa ajabu na sio kupofua watu wengine kwa ngozi zisizo zao!Tamaa inaua wadau...
 
Hivi inakuaje mwanamke anaondoka nyumbani kwake anamuaga mume wake ambae ni mzuri as in hamnyanyasi na anajitahidi siku zote kumfanyia mke yaliyo mema..alafu anaenda kukutana na kimada wake ambae nae ni mume wa mtu ambae nae mke wake anajitahidi kumfanyia yaliyo mema?Yani wote wanavunja ahadi zao kwanza kwa kutoka nje ya ndoa zao alafu wanafikia kutamani mpaka kutembea na mume/mke wa mwingine!Watu hawa ambao kuna watu wanawaangalia kama 'rolemodels' kwenye maswala ya maisha tuwachukulieje?
Nimeuliza Lizzy una mume ili tuone tutachangia vipi maana unaweza ukawa unaizungumzia ndoa kinadharia zaidi. Kama umeolewa una muda gani ndani ya ndoa? Ukitaka kumlaumu mtu unatakiwa kwanza uvae viatu vyake ndo uweze kukosoa ama kusifia
 
Sasa kama mtu hajaridhika na mambo ya kidunia kwanini amtulize mwenzake huku yeye akitapa tapa kila kona ya mji?Kwanini asisubiri atakapokua tayari kutulia?
Hulka ya mtu kama anayo haiwezi kubadilika hata kama akiolewa wengine wanaoa/kuolewa kutimiza wajibu tu akiingia ni yule yule atapata kila kitu lakini bado atakuwa kiruka njia tu.
 
Nimeuliza Lizzy una mume ili tuone tutachangia vipi maana unaweza ukawa unaizungumzia ndoa kinadharia zaidi. Kama umeolewa una muda gani ndani ya ndoa? Ukitaka kumlaumu mtu unatakiwa kwanza uvae viatu vyake ndo uweze kukosoa ama kusifia

Sidhani kama kuna ulazima wa mtu kuwa benki aone pesa kibao wakati ana shida kusema kwamba wizi sio mzuri!
 
Bado!Vipi kwani?
Hupaswi kulaumiwa kwa swali ulilouliza. Ila kwa ufupi kila mtu atokaye nje ya ndoa hutoka kwa sabababu zake. Hivyo ni ngumu kulijibu swali lako kwa ujumla. Lakini jibu sahihi ni kwamba. Nakushauri kabla hujashangaa sana na haya olewa kwanza halafu baada ya miaka 10-15 ya ndoa recall hili swali naamini utakuwa na jibu sahihi.
 
Grandpa DC hayo mambo ya kuchunguza nyama za kila bucha ndo haswa hua zinaniacha hoi...kwanini ununue sehemu moja kama bado una mawazo na hisia kwamba bucha la mtaa wa pili inaweza kua bora zaidi!Kwanini asionje kwanza mpaka atakaporidhika nafsini mwake kwamba utumbo ni mzuri kuliko maini na steak?Kama haupo tayari kuwa na kutulia na mtu mmoja usioe wala usiolewe.Kusema watu wanaoa kutimiza majukumu hata kua mwaminifu ni jukumu linajuofuatana na ndoa...kama hilo hawaliwezi ndoa ya kazi gani?
 
Nimeuliza Lizzy una mume ili tuone tutachangia vipi maana unaweza ukawa unaizungumzia ndoa kinadharia zaidi. Kama umeolewa una muda gani ndani ya ndoa? Ukitaka kumlaumu mtu unatakiwa kwanza uvae viatu vyake ndo uweze kukosoa ama kusifia
Kumbe mpaka uwe umeoa/kuolewa ndio unaweza kuzungumzia ndoa, nilikuwa sijui kwa style hii kazi ipo
 
Kumbe mpaka uwe umeoa/kuolewa ndio unaweza kuzungumzia ndoa, nilikuwa sijui kwa style hii kazi ipo
Kuna tofauti kubwa kati ya kuzungumza na kutenda unachozungumza. Wengi ya watu kabla ya kuoa walijiuliza maswali haya na mengine ila majibu yake wanayapata wakati wameoa. Kuna mtu alijiuliza inakuwaje mume na mke wanaachana hakupata jibu zaidi ya porojo ila baada ya kuoa kama 5yrs wakaachana na mkewe akawa ana majibu yote. kwa hiyo hili nalo lina jibu sahihi wakati ukiwa ndani ya ndoa ingawaje kila mtu akatoa majibu sasa hivi lakini 99% si sahihi.
 
Hupaswi kulaumiwa kwa swali ulilouliza. Ila kwa ufupi kila mtu atokaye nje ya ndoa hutoka kwa sabababu zake.

Hizo sababu ni zipi haswa?Kama ndoa imekua chungu kwanini wasiachane?Utasikia watu wanasema kuachana sio suluhisho...kutoka nje ndio suluhisho?Alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe...mbona kutoka nje ya ndoa sio sawa na wanatoka?Unless watu wanatumiana tu..zipo njia za kurekebisha mambo na yakishindikana kabisa kila mtu ajue njia yake!
 
Back
Top Bottom