Lizzy.....hope you had a wonderful easter
Maisha ni kitu kigumu sana kukielewa hasa katika nyanja ya mapenzi Dada yangu. Kutokana na post yako ni wazi kuwa unawafahamu fika whoever unayemzungumzia BUT sidhani kama unawafahamu kwa kiasi hicho cha kujua wenzi wao ni wema, wazuri n.k kwa sababu aliyeko ndani ya chungu kile ndiye ajuaye ukali wa moto unaopikia. So kusema kuwa mume wa mwanamke mtokaji ni mzuri, mwema n.k. we need to be cautioned kidogo.
Pili kuna mtu alishasema kuwa kuolewa/oa si mwisho wa kupenda. Ni utashi wa binadamu na utaendelea tu kuwa hivyo so kuridhika na uliye naye ni azi kidogo. Na si kweli kuwa waliooa/olewa hawapendi tena bali tunakuwa restricted na taratibu za ndoa kuwa ukishaoa/olewa huruhusiwi kupenda tena japo ni against human nature. So watu tunalazimika kuabide and wherever there is this condition inategemea na uwezo wa mtu wa kujicontrol kuzuia kupenda nje so tegemea kuna wanaoweza na wale wasioweza.....ni maumbio yetu.
Lakini pia sikatai kuwa kuna mmomonyoko wa maadili kuwa tamaa zinatuzidi na tunajikuta tunashindwa abstain. ila panapohusika na tamaa si rahisi ukawakuta hawa wawili wakadumu kwa muda mrefu as watatamani tena sehemu nyingine na safari ikaendelea. Maisha ya mahusiano ni magumu kwa kweli.
Mwisho kwenye suala la kuwa role models na wanaowapreachia kuwa wema wakati wao ni waovu............tunahubiriwa kila siku kuwa kutende kwa kadri ya mafundisho yao na si kwa matendo yao.......na hii haiko katika mahusiano tu, hata kidini ni mara ngapi tunakuwa na wahubiri au viongozi wa dini wenye mambo ya kidunia but tunashauriwa kutenda yale wanayotuhubiria na si yale wanayoyatenda.
Happy Easter bi dada