Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Mawazo kama haya ndo yanasababisha watu kuona kwamba hamna utofauti Kati ya CCM na upinzani. Una uhakika gani kwamba ni CDM wote hawataki mabadiliko ya mwenyekiti?
 
Kama Chadema wanaona ni sawa kuongozwa na mwenyekiti huyohuyo miaka nenda rudi wanaonaje ajabu JPM akiongoza miaka saba saba.
 
Mawazo kama haya ndo yanasababisha watu kuona kwamba hamna utofauti Kati ya CCM na upinzani. Una uhakika gani kwamba ni CDM wote hawataki mabadiliko ya mwenyekiti?
Chadema zaidi ya 92% wenye akili timamu hatuitaji mabadiliko ya mwenyekiti.Kama huamini weka poll tupige kura hapa.
Mawazo kama haya ndo yanasababisha watu kuona kwamba hamna utofauti Kati ya CCM na upinzani. Una uhakika gani kwamba ni CDM wote hawataki mabadiliko ya mwenyekiti?
 
Lengo la CCM na serikali ni kuona Chadema ikipata mwenyekiti dhaifu dizaini ya kina Lipumba, Cheyo, Mrema na mama Mgwhira ili wapate chance ya kukisambaratisha.

Mbowe ana msimamo, ni mpinzani halisi, kimsimamo hana tofauti na Seif. Ana hekima, ana busara hakurupuki anajua nini chama chake na wafuasi wake wanataka, hana jaziba wala visasi kama mwenyekiti wa upande wa pili. Kuongezea hapo Mbowe hana njaa za kijinga ana biashara zake, hanunuliki. Wamejaribu kuharibu mali zake wakafikiri atalegeza msimamo, TRA wamembambikia kodi kalipa, NHC wamebomoa Bilicanas wakafikiri ndiyo biashara yake pekee.

Mbowe sio Mrema wa kudanganywa kwa cheo mbuzi, kwa Mbowe CCM watakesha sana na naomba wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema uchaguzi utakapofika wamchague tena kwa kura zaidi ya alizopata tuwashangaze mahasimu wake.
 
Ccm wanataman tupate mwenyekiti kama docta mihogo ili ndoto yao ya chadema kufa itimie.
 
Siyo CCM Wala CDM iliyo mali ya mtu,ruzuku ni mali ya watanzania wote. Kama hupendi kuhojiwa sajili saccos yako uiendeshe unavyotaka.
 
cdm bhana ...bas kila chama kipambane na hali tuone nani atakua wa kwanza kulalamika
 
Hili jambo huwa silielewi kabisa. Kweli Mbowe kama binadamu ana madhaifu yake, lakini inakuwaje ni CCM ndiyo wanataka kuweka ukomo wa uenyekiti wa Mbowe CHADEMA?

Yaani ni kama Wamarekani waseme ni kwa nini wajerumani wanaendelea kuchagaua Angela Merkel kuwa Kansela wao. CCM kuhusu Mwenyekiti wa Taifa hakuna mahali kwenye katiba yao pamewekwa ukomo wa muda, bali wanabadilishana kwa kutegemea "Tamaduni" ya chama hicho na wala si kwa uchaguzi kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho hakuna kugombea nafasi ya mwenyekiti Taifa.

Sasa chama ambacho huwa hakifanyi kabisa uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa, kinakuwaje na nguvu ya kimaadili kuwaambia CHADEMA wabadilishe Mwenyekiti wao Taifa? Kwani kwenye Katiba ya CHADEMA kuna kipengele kinakataza mtu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa zaidi ya mara moja?
Ni jambo baya, na ni utamaduni mbovu kiongozi mmoja kukaa madarakani muda mrefu...ndo mambo ya kimobutu, kimugabe, etc.
Mtu ambaye hataki kuachia madaraka ya chama zaidi ya miaka 10, hawezi kuwa na dhamira ya kuiacha ikulu baada ya awamu yake ya miaka 5 kuisha.
 
Nuerere aliongoza miaka zaidi ya 20 pamoja na ile ya TANU ili ajenge chama. Mandela hivo hivo hata akiwa jela bado alikuwa kiongozi ANC. Mwanzo mzuri wa kila chama lazima mtu shupavu na mwenye hali awe kiongozi la sivyo chama hufa.
Mbona hawamsemi Mrema?
Wanataka chadema iweke ombaomba kama mrema?
 
Mimi binafsi sifurahii kiongozi kukaa madarakani muda mrefu ila nina uhakika 100% kama mbowe angeachia madaraka ndani ya miaka 10 ya uongozi wake Leo tusingekuwa na chadema. Lakini binafsi bado najua mtu pekee anayeweza kumrithi mbowe ni TL. Sababu kubwa kwangu ni hizi. Kwanza mbowe anajua uchungu was CDM kama mama mzazi anavyojua uchungu wa kujifungua, mbowe kaanza na chama akiwa kijana, katumwa katumika, kapitia changamoto na kaimarishwa na changamoto nyingi na hujuma za chama tawala. Pili mbowe ana maisha, hawezi kununuliwa wala kuhongwa na ndiyo maana ccm wameshindwa kumnyamazisha. Mbowe nadhani ndiye mfanyabiashara safi nchi hii maana wangeshamaliza. Lakini TL ni mpinzani kwa damu na jasho, TL hawezi kukaa na maccm kujadiliana kuhusu kuuza chama, ni mtu mwenye msimamo wa dhati na kutoka moyoni hawezi kuuza chama. Viongozi wengine nao ni wazuri ila bado ni vijana wanatafuta maisha na bado wanaweza kubabaishwa kwa pesa kama professor fulani. KWANGU MIMI NINGEPENDEKEZA MBOWE AMALIZE NA MHESHIWA RAIS 2020/2025.
 
Wapo wengi tu na hakuna siku Mbowe kalazimisha kushinda bali huwashinda anaoshindana nao. Kama kura zinapigwa na yeye anashinda shida iko wapi?
heeh kumbe kuna watu waligombea uenyekiti chadema dhidi ya mbowe??? haya ni maajabu, nataman uanzishe post alafu ututajie hao waliogombea uenyekiti na mbowe
 
kwa akili hizi za wanachama, acha mbowe aendelee tu kuwa mwenyekiti
 
Mtu yeyote ambaye ahongeki ni mtihani mzito kwa mhongaji.
Ina maana katika wanachama woooote wa CDM hakuna mwingine asiyehongeka zaidi ya Mbowe? Kama ni hivyo basi hamna chama hapo. Siku mkipewa madaraka mtapata wapi mawaziri na viongozi wasiohongeka?
 
Back
Top Bottom